WAZIRI SIMBACHAWENE ATOA WITO KWA VIONGOZI KUSIKILIZA MALALAMIKO YA WATUMISHI WA UMMA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, March 3, 2025

WAZIRI SIMBACHAWENE ATOA WITO KWA VIONGOZI KUSIKILIZA MALALAMIKO YA WATUMISHI WA UMMA



Na Okuly Julius _DODOMA


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, GEORGE SIMBACHAWENE, amesema Ofisi hiyo inaendelea kupokea malalamiko ya watumishi wanaokataliwa kupokelewa katika vituo walivyohamishiwa au kuajiriwa, wale wanaokutana na unyanyasaji wa kijinsia, na ucheleweshaji wa haki stahiki za kiutumishi.

Waziri SIMBACHAWENE amesema hayo jijini Dodoma wakati akizungumza katika kikao kazi cha wakuu wa idara za serikali zinazojitegemea, watendaji wakuu wa wakala wa serikali, watendaji wakuu wa mashirika, taasisi za umma, wakurugenzi wa majiji, manispaa na miji na wakurugenzi watendaji wa halmashauri za wilaya, ikiongozwa na Kaulimbiu isemayo "Matumizi sahihi ya Rasilimaliwatu kwa Maendeleo Endelevu ya Taifa" .

"bado Utumishi wa Umma unakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kutokuzingatiwa kwa Sheria, Kanuni, Taratibu, Miongozo na Maelekezo yanayosimamia masuala mbalimbali ya Kiutawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu. Kumekuwa na ukiukwaji wa Sheria, Kanuni, Taratibu na Miiko ya kazi katika Utumishi wa Umma ikiwemo matumizi mabaya ya madaraka na Ofisi,

Na kuongeza kuwa "Changamoto zingine zinazojitokeza ni pamoja na kufanya kazi pasipo kuzingatia mipaka na mamlaka ya kisheria, baadhi ya Watendaji Wakuu wa Taasisi kufanya maamuzi pasipo kuzingatia ushauri wa kitalaamu kutoka kwa Watumishi walio chini yao lakini pia hata walio juu yenu kama vile Bodi zenu, Wizara Mama na Mamlaka za Tawala za Mikoa (RS), "amesema Waziri Simbachawene

Katika hatua nyingine Waziri SIMBACHAWENE amesema kuwa Tanzania ni nchi tajiri kwani imejaaliwa rasilimali Watu ambao wanatakiwa kuhakikisha wanasimamia vizuri rasilimali nyingine ili kuweza kuleta tija kwa Taifa.

"Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma ni Rasilimali ya thamani na mojawapo ya nyenzo muhimu ambayo Serikali inaitumia kuwafikia Wananchi wake katika kutoa huduma muhimu za kijamii na kiuchumi ili kuleta usawa na kukuza ustawi katika jamii nzima"

Na kuongeza kuwa "kutokana na umuhimu wa rasilimali hii, ninyi kama Watendaji wakuu katika Taasisi zenu mnawajibu na dhamana kubwa ya kuhakikisha matumizi sahihi ya Rasilimali hiyo muhimu na ya thamani ambayo inayosimamia Rasilimali nyingine ili ziweze kuleta tija katika kutoa huduma bora kwa Umma na kuchangia ustawi na maendeleo ya jamii kwa ujumla,"ameeleza Simbachawene

Amesema katika bajeti ya mwaka wa fedha 2023/2024 Serikali kupitia Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imewapandisha vyeo watumishi laki mbili thelathini na mbili elfu, mia tisa ishirini na saba (232,927) na kuwabadilisha Kada Watumishi elfu kumi na moja na kumi na nane (11,018).

Aidha, katika Mwaka wa fedha 2024/25 amesema Serikali inatarajia kupandisha vyeo Watumishi laki mbili kumi na tisa elfu na Arobaini na mbili (219,042) na kuwabadilisha Kada Watumishi elfu sita mia tisa na kumi (6,910).

Vilevile, Serikali imetoa nyongeza ya mwaka ya mshahara kwa watumishi wake na itaendelea kuboresha maslahi ya watumishi kulingana na uwezo wa uchumi.

"Ni jukumu lenu kama Waajiri wa watumishi wa Umma kuendelea kuwasimamia watumishi walio chini yenu kwa kuwaelimisha kuhusu haki na wajibu wao ili wanapodai haki wajue kuwa kuna wajibu wanapaswa kuwa wametekeleza," amesisitiza Simbachawene

Naibu Waziri wa Ofisi hiyo, DEUS SANGU ameeleza uwepo wa changamoto kwa baadhi ya Waajiri wanaowanyima kwa makusudi watumishi wao baadhi ya stahiki zao ikiwemo za uhamisho.









No comments:

Post a Comment