MWENYEKITI ACT WAZALENDO TAIFA AJITOSA KUWANIA URAIS ZANZIBAR - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Sunday, April 13, 2025

MWENYEKITI ACT WAZALENDO TAIFA AJITOSA KUWANIA URAIS ZANZIBAR


Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Taifa Othman Masoud Othman amechukua fomu ya kugombea Urais wa Zanzibar huku akiomba Wanachama kumpa ridhaa akiamini uwezo mkubwa alionao kuongoza Zanzibar baada ya uchaguzi mkuu mwezi October 2025.

Othman amechukua fomu hiyo leo April 14, 2025 ofisi ndogo za makao makuu ya Chama Vuga mjini Unguja, akishuhudiwa na Viongozi mbalimbali wa Chama hicho. Amesema hatua ya kuchukua kwake fomu imekuja baada ya kuona ipo haja ya kuleta mabadiliko ya kiuongozi Zanzibar na wakiamini Chama cha ACT Wazalendo ndio mbadala wa kuiondoa CCM madarakani.

Kwa upande wake Naibu katibu wa Chama hicho Zanzibar Omar Ali Shehe amesema hamasa kubwa ya uchukuaji wa fomu kugombea nafasi tofauti za Chama imeongezeka tangu kuanza kwa zoezi hilo.

Amesema pamoja na kuchukua kwake fomu Mwenyekiti wa Chama Othman Masoud Othman ambae ni Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar bado milango ipo wazi kwa yoyote anaetaka kuchukua fomu kuomba ridhaa ya kugombea Uraisi kupitia chama hicho.


“Kuchukua fomu kwa Mwenyekiti wetu hakuna maana ya kuzuia wengine milango ipo wazi kila mtu ana haki ya kuchukua fomu”

No comments:

Post a Comment