KAMATI YA BUNGE YA NUU YAKAGUA UJENZI WA HOSPITALI YA KANDA YA JESHI LA MAGEREZA - MSALATO DODOMA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Sunday, April 13, 2025

KAMATI YA BUNGE YA NUU YAKAGUA UJENZI WA HOSPITALI YA KANDA YA JESHI LA MAGEREZA - MSALATO DODOMA



Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) ikiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Vicent Mbogo (Mb) imetembelea na kukagua Ujenzi wa Hospitali ya Kanda ya Jeshi la Magereza iliyopo Msalato Dodoma.

Kamati hiyo imekagua ujenzi huo, leo tarehe 13 Aprili 2025 ambapo iliambatana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa pamoja na Kamishna Jenerali wa Magereza, CGP Jeremiah Y. Katungu.

Akizungumza baada ya kukagua Ujenzi wa Hospitali hiyo, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya NUU, Mhe. Vicent Mbogo (Mb) ameipongeza Serikali kupitia Jeshi la Magereza kwa kuendelea kutekeleza miradi ya afya ambayo imekuwa msaada mkubwa kwa kutoa huduma za afya kwa Maafisa, askari, wafungwa na maabusu pamoja na wananchi wanaozunguka maeneo hayo.

Aidha, Mhe. Mbogo ametoa wito kwa Jeshi la Magereza kuhakikisha linapima maeneo yake na kuwa na hatimiliki ya ardhi ili kuepuka migogoro na uvamizi wa watu wanaozunguka maeneo hayo.

Kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa amesema Wizara inaendelea kufuatilia kwa ukaribu ili kuhakikisha fedha zinazotengwa kupitia Hazina kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo zinatolewa kwa wakati kulingana na mpango kazi.

Kadhalika, Bashungwa amelitaka Jeshi la Magereza kuwa na Mkakati mzuri wa matumizi ya ardhi ikiwa ni pamoja na kupima eneo la Magereza Msalato lenye hekari 7,000 na kuwa na hatimiliki ili kulinda eneo hilo dhidi ya uvamizi

Awali, Kamishna Jenerali wa Magereza, CGP Jeremiah Y. Katungu amesema Jeshi la Magereza linaendelea kutenga fedha kupitia bajeti ili kuendeelea na kazi ya ujenzi kwa ajili ya kukamilisha majengo ya awali ili hospitali hiyo iaze kutoa huduma za awali.

Mradi wa Hospitali hiyo umekadiriwa kugharimu jumla ya Shilingi 26,157,140,830 hadi kukamilika na utahusisha ujenzi wa majengo 31 ya kutolea huduma za Afya.









No comments:

Post a Comment