Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Dodoma Comrade Charles Mamba Azindua Baraza la Wazee wa CCM Kata ya Kilimani - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, April 14, 2025

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Dodoma Comrade Charles Mamba Azindua Baraza la Wazee wa CCM Kata ya Kilimani


Na Barnabas Kisengi, Dodoma


Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Kilimani jijini Dodoma kimezindua Baraza la Wazee wa Chama hicho katika kata hiyo, ikiwa ni hatua muhimu ya kuimarisha uongozi na maadili ndani ya chama.

Akizindua baraza hilo, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Dodoma, Comrade Charles Mamba, amesema kuwa uwepo wa baraza hilo utaleta tija kubwa kwa chama, viongozi pamoja na wanachama wa CCM katika kata ya Kilimani.

“Hili Baraza mmelizindua wakati muafaka, maana Kilimani tunayoiijua sisi hapa katikati ilianza kupoteza maadili kwa viongozi na wanachama. Sasa hili Baraza la Wazee hakikisheni mnairejesha Kilimani ilipokuwa, kwa kuwa Kilimani ndiyo imebeba sura ya kuwa na viongozi wengi wa serikali na chama kuishi hapa,” amesema Comrade Mamba.

Ameongeza kuwa baraza hilo litahakikisha masuala ya maadili yanapewa kipaumbele kwa viongozi na wanachama wote wa CCM katika kata ya Kilimani.

Awali, akisoma risala ya wazee, Mwenyekiti wa Baraza la Wazee kata ya Kilimani, Mzee Chambasi, amesema changamoto kubwa inayowakabili wazee wa kata hiyo ni suala la afya, ambapo wazee wengi hawana bima ya afya. Pia, amesema baadhi ya mitaa kama Chinyoyo na Image bado inakabiliwa na changamoto ya miundombinu ya barabara, hasa katika kipindi cha mvua, hali inayosababisha mitaa hiyo kukosa mawasiliano mazuri ya barabara.


Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini ambaye pia ni Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Peter Mavunde, amekipongeza Chama cha Mapinduzi kata ya Kilimani kwa kuunda Baraza hilo kwa mujibu wa katiba ya CCM.

Mhe. Mavunde amewataka wazee wote waandikishwe vizuri ili kujua idadi ya wale wasio na kadi za bima ya afya, na kusema kuwa atahakikisha anawapatia bima hizo.

Aidha, Mhe. Mavunde amegusia changamoto ya miundombinu ya barabara ya mtaa wa Chinyoyo ambayo imekuwa ikiwapa shida wananchi kwa muda mrefu. Amesema kuwa katika bajeti ya mwaka 2025/2026 barabara hizo zimetengewa fedha na zitajengwa kwa viwango vizuri kupitia TARURA.

“Nimekuwa nikiumia sana kwa barabara za mtaa wa Chinyoyo jinsi zinavyowatesa wananchi, lakini katika bajeti yetu ya mwaka huu tumezitengea fedha ili zitengenezwe kwa ubora kupitia TARURA,” amesema Mavunde.

Ameongeza kuwa tangu nchi ipate uhuru, kata ya Kilimani haijawahi kuwa na shule ya msingi wala ya sekondari, lakini sasa tayari ameanzisha ujenzi wa shule ya msingi ambao uko katika hatua za mwisho. Hivi karibuni, ujenzi wa shule ya sekondari utaanza pia.

No comments:

Post a Comment