
Na Okuly Julius _ DODOMA
Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Hamad Hassan Chande, amesema kuwa Serikali kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeendelea kutoa elimu ya kodi kwa walipakodi wote wakiwemo wajasiriamali wanawake kupitia vikundi vyao mbalimbali.
Akijibu swali la Mheshimiwa Janeth Elias Mahawanga (Viti Maalum) Bungeni leo Aprili 11, 2025, kuhusu mpango wa Serikali kuanzisha madarasa ya elimu kwa mlipa kodi kupitia vikundi vya wanawake wajasiriamali, Mhe.Chande amesema TRA imekuwa ikishirikiana na taasisi kama Tanzania Women Chamber of Commerce (TWCC) na makundi mengine ili kuwajengea uwezo katika masuala ya ulipaji kodi.
Amesema kuwa TRA itaendelea kushirikiana na wizara husika ili kuimarisha mawasiliano na mitandao ya wanawake wajasiriamali kwa lengo la kufikisha elimu hiyo kwa ufanisi zaidi na kuchochea shughuli zao za kiuchumi.
No comments:
Post a Comment