
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana, amesema kuwa hadi Aprili 2025, jumla ya tani 1,321.35 za asali zenye thamani ya Shilingi 15,856,164,000 zimeuzwa nje ya nchi, sawa na ongezeko la asilimia 206.9 ikilinganishwa na tani 430.61 yenye thamani ya Shilingi 5,167,332,000 zilizouzwa kwa kipindi kama hicho mwaka 2024.
Wazira Chana ameyasema hayo leo Mei 19,2025 Bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha Hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2025-2026.
Amesema mafanikio hayo yamepelekea Shirika la Wafugaji Nyuki Duniani kumteua Tanzania kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Wafugaji Nyuki duniani (APIMONDIA) utakaofanyika mwaka 2027, utakaohudhiwa na zaidi ya washiriki 4,000 kutoka sehemu mbalimbali za dunia.
No comments:
Post a Comment