
Wizara ya Maliasili na Utalii imesema kuwa Tanzania imeendelea kuongoza Afrika na duniani kwa kuwa na idadi kubwa ya wanyamapori, ikiwa ni pamoja na simba wapatao 17,000.
Hayo yamesemwa leo Bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Wizara hiyo Balozi Dkt. Pindi Chana wakati akiwasilisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2025-2026
Aidha, Tanzania inaongoza barani Afrika kwa kuwa na nyati wapatao 225,000 na chui 24,000. Takwimu zinaonesha pia kuwa idadi ya faru weusi imeongezeka kutoka 163 mwaka 2021 hadi 263 mwaka 2025, sawa na ongezeko la asilimia 61.
Wazira chana amesisitiza kuwa juhudi za uhifadhi zimezaa matunda ambapo matukio ya ujangili wa tembo yamepungua kwa takriban asilimia 90, ikiwa ni mafanikio makubwa ya Serikali katika kulinda rasilimali za taifa.
No comments:
Post a Comment