Na Mwandishi Wetu, Tabora
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Mhe. William Lukuvi, amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika ibada maalum ya kuwekwa wakfu kwa Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Tabora, Mhashamu Josephat Jackson Bududu.
Ibada hiyo ya Misa Takatifu imefanyika leo, Mei 25, 2025, katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Theresia, Jimboni Tabora, na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, Kanisa na waumini kutoka maeneo tofauti.
Katika hotuba iliyosomwa kwa niaba ya Rais Samia, Mhe. Lukuvi amempongeza Askofu Bududu kwa kuteuliwa kushika nafasi hiyo, akieleza kuwa Serikali inaendelea kuthamini mchango wa taasisi za dini katika kuimarisha maadili, amani na maendeleo ya jamii.
Sherehe hiyo imehudhuriwa pia na viongozi wa madhehebu mbalimbali, ikionyesha mshikamano wa kidini na kijamii katika mkoa wa Tabora.
No comments:
Post a Comment