BARAZA JIPYA LA WAFANYAKAZI LA WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI LAUNDWA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, May 19, 2025

BARAZA JIPYA LA WAFANYAKAZI LA WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI LAUNDWA



Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji,akizungumza wakati wa mkutano wa baraza la wafanyakazi wa Wizara hiyo uliofanyika leo Mei 19, 2025 katika ukumbi wa Mabeyo – Complex jijini Dodoma. Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi ambaye ni mwenyekiti wa baraza hilo Prof. Riziki Shemdoe,akizungumza wakati wa mkutano wa baraza la wafanyakazi wa Wizara hiyo uliofanyika leo Mei 19, 2025 katika ukumbi wa Mabeyo – Complex jijini Dodoma.

Sehemu ya washiriki wakimsikiliza Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (hayupo pichani) wakati wa mkutano wa baraza la wafanyakazi wa Wizara hiyo uliofanyika leo Mei 19, 2025 katika ukumbi wa Mabeyo – Complex jijini Dodoma.

Na.Mwandishi Wetu

Baraza jipya la wafanyakazi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi limeundwa kwa lengo la kuwashirikisha wafanyakazi wa Wizara hiyo katika utekelezaji wa shughuli za Serikali na ushirikiano, kuishauri Wizara juu ya ufanisi wa kazi na hatua zinazofaa kuchukuliwa ili kuimarisha utoaji huduma.

Akizungumza katika mkutano uliofanyika leo Mei 19, 2025 katika ukumbi wa Mabeyo – Complex jijini Dodoma Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji amesema baraza hilo linapaswa kushauri Wizara juu ya mambo muhimu yanayohusu Haki, Wajibu na Maslahi ya wafanyakazi ili kuleta ufanisi na tija katika utekelezaji wa malengo ya Wizara hiyo.

“tunapaswa kulitumia baraza hili kama jukwaa muhimu la kutolea maoni, kujadili masuala yanayowahusu wafanyakazi na kutafuta suluhu ya changamoto mbalimbali zinazoikabili Wizara yetu”

Ameongeza kuwa katika mwaka wa Fedha 2025/2026 Wizara imejiwekea vipaumbele ambavyo ni Kuimarisha afya ya mifugo na viumbe maji, mifumo ya utambuzi wa mifugo, kuimarisha uongezaji thamani na masoko,pamoja na biashara ya mazao ya mifugo na uvuvi.

Pia Kuimarisha ulinzi na usimamizi wa rasilimali za Mifugo na Uvuvi kwa kuanzisha vyombo maalum vya utendaji kwa ajili ya kusimamia na kulinda rasilimali za wizara hiyo na kuboresha vituo vya ulinzi na usimamizi wa rasilimali zake na Kuimarisha utafiti, mafunzo na huduma za ugani katika sekta hiyo kuimarisha uwezo wa Taasisi za Utafiti na Mafunzo ya Mifugo na Uvuvi.

Kwa Upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi ambaye ni mwenyekiti wa baraza hilo Prof. Riziki Shemdoe amesema baraza hilo linaridhaa ya watumishi wote wa Sekta hiyo na kutakuwa na mjadiliano ya ajenda ikiwemo na ajenda ya bajeti.

Baraza la kwanza la fungu 99 limeundwa baada ya muunganiko wa sekta hizo mbili kwa kuzingatia kanuni na sheria ya mashauriano katika utumishi wa umma ya mwaka 2003 (the Public Service Negotiating Machinery, Act 2003) XXXX

No comments:

Post a Comment