MALIASILI NA UTALII KUKUSANYA SHILINGI TRILIONI 1.2 - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, May 19, 2025

MALIASILI NA UTALII KUKUSANYA SHILINGI TRILIONI 1.2



Katika mwaka 2025/2026, Wizara ya Maliasili na Utalii inatarajia kukusanya maduhuli ya zaidi ya Sh trilioni 1.184.

Haya yamebainishwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt.Pindi Chana (Mb wakati wa kuwasilisha mpango wa mapato na matumizi ya wizara na taasisi zake kwa mwaka 2025/26.

Amesema kuwa fedha hizo zimepagwa kukusanywa kutoka kwenye idara na taasisi zake.

Kwa mwaka 2024/25, Wizara iliidhinishiwa kukusanya jumla ya Sh bilioni 968.8 na kati ya fedha hizo, Sh bilioni 755.42 zinakusanywa na Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Taasisi za TANAPA, NCAA na TAWA na kuwasilishwa Mfuko Mkuu wa Serikali kupitia TRA na Sh bilioni 213.42 zinakusanywa na Wizara kutokana na vyanzo vya mapato kutoka Idara Wizara kutokana na Idara, Mifuko na Taasisi zake kupitia mfumo wa MNRT Portal.

Amesema hadi kufikia Machi 2025, Wizara imekusanya jumla ya Sh bilioni 877.387sawa na asilimia 90.56 ya lengo la makusanyo.

Kati ya fedha hizo, Shilingi bilioni 710.93 zimekusanywa na Wizara kutokana na vyanzo vya Taasisi za TANAPA, NCAA na TAWA.

Aidha kiasi cha Shilingi bilioni 166.458 zimekusanywa na Wizara kutokana na Idara, Mifuko na Taasisi zake kupitia mfumo wa MNRT Portal.



No comments:

Post a Comment