BASHUNGWA ASHIRIKI BARAZA LA MAWAZIRI WA MASUALA YA AMANI NA USALAMA WA EAC, UGANDA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, May 23, 2025

BASHUNGWA ASHIRIKI BARAZA LA MAWAZIRI WA MASUALA YA AMANI NA USALAMA WA EAC, UGANDA


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa (Mb), ameshiriki Mkutano wa Tisa wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Masuala ya Amani na Usalama wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, uliofanyika leo, tarehe 23 Mei 2025, jijini Entebbe, nchini Uganda.

Mkutano huo muhimu, uliolenga kuimarisha ushirikiano wa kikanda katika masuala ya amani na usalama kwa kujadili changamoto za kiusalama zinazozikabili nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na kuweka mikakati ya pamoja ya kukabiliana nazo, ulitanguliwa na mkutano wa ngazi ya Makatibu Wakuu na Wataalamu ulioanza tarehe 19 hadi 22 Mei 2025.

Mawaziri wamejadili na kukubaliana kwa pamoja kuhusu utekelezaji wa masuala mbalimbali muhimu, ikiwemo kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kikanda katika kukabiliana na uhalifu unaovuka mipaka, kuboresha usimamizi wa mipaka, kuboresha matumizi ya vitambulisho vya taifa, na kukamilisha mchakato wa kuandaa utaratibu wa pamoja wa usimamizi wa masuala ya wakimbizi.

Katika mkutano huo, ujumbe wa wataalamu kutoka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania umeongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Dkt. Maduhu Kazi, ambapo aliambatana na maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani, Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Idara ya Uhamiaji, na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).

No comments:

Post a Comment