MAFUNZO YA MFUMO WA D- Fund MIS ULIOBORESHWA YATOLEWA KWA WADAU - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Sunday, May 18, 2025

MAFUNZO YA MFUMO WA D- Fund MIS ULIOBORESHWA YATOLEWA KWA WADAU


Mchumi Mkuu kutoka Idara ya Fedha za Nje, Wizara ya Fedha, Bw. John Kuchaka, akifungua kikao kazi kwa washiriki kutoka Wizara, Taasisi na Idara zinazojitegemea kuhusu Mfumo wa D-Fund Management System (D-Fund MIS) ulioboreshwa unaotumika kuratibu utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayofadhiliwa kwa fedha za Washirika wa Maendeleo, jijini Dodoma.



Mratibu wa Mafunzo ya Mfumo wa D-Fund Management System (D-Fund MIS) ulioboreshwa unaotumika kuratibu utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayofadhiliwa kwa fedha za Washirika wa Maendeleo, Bi. Selina Mwakipesile, akitoa maelezo kuhusu umuhimu wa kuzingatia matumizi sahihi ya Mfumo huo, wakati wa mafunzo kwa washiriki kutoka Wizara, Taasisi na Idara zinazojitegemea, jijini Dodoma.



Mchumi kutoka Idara ya Fedha za Nje Wizara ya Fedha, Bw. Fredrick Makere, akitoa mada kuhusu maeneo ya mfumo wa D-Fund Management System (D-Fund MIS) yaliyo boreshwa, kwa washiriki kutoka Wizara, Taasisi na Idara zinazojitegemea, jijini Dodoma.



Mtaalam wa Mifumo kutoka Idara ya Usimamizi wa Mifumo ya Fedha na Tehama, Wizara ya Fedha, Bw. George Nguvava, akieleza urahisi wa matumizi ya Mfumo wa D-Fund Management System (D-Fund MIS) ulioboreshwa kwa washiriki wa mafunzo kutoka Wizara, Taasisi na Idara zinazojitegemea, jijini Dodoma.



Mshiriki wa Mafunzo ya Mfumo wa D-Fund Management System (D-Fund MIS) ulioboreshwa unaotumika kuratibu utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayofadhiliwa kwa fedha za Washirika wa Maendeleo, Bw. Eli Barongo akiuliza swali kuhusu maeneo ya Mfumo yaliyoboreshwa, wakati wa mafunzo kuhusu mfumo kwa washiriki kutoka Wizara, Taasisi na Idara zinazojitegemea, jijini Dodoma.



Mchumi kutoka Idara ya Fedha za Nje, Wizara ya Fedha, Bw. Dastan Komba, akitoa mada kuhusu changamoto za mfumo wa D-Fund Management System (D-Fund MIS) kabla haujaboreshwa wakati wa mafunzo ya mfumo huo kwa washiriki kutoka Wizara, Taasisi na Idara zinazojitegemea, jijini Dodoma.




Baadhi ya Washiriki wa Mfumo wa D-Fund Management System (D-Fund MIS) ulio boreshwa, kutoka Wizara, Taasisi na Idara zinazojitegemea, wakifuatilia mada zinazowasilishwa kuhusu mfumo huo, jijini Dodoma.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano, Wizara ya Fedha, Dodoma)

Na. Josephine Majura na Peter Haule, WF, Dodoma


Wizara ya Fedha imefanya mafunzo ya Mfumo wa D-Fund Management System (D- Fund MIS) ulioboreshwa unaotumika kuratibu utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayofadhiliwa na Washirika wa Maendeleo.

Akifungua mafunzo hayo jijini Dodoma, Mchumi Mkuu kutoka Idara ya Fedha za Nje, Bw. John Kuchaka, alisema kuwa Wizara ya Fedha imefanya maboresho ya Mfumo wa D-Fund ili kuongeza tija zaidi kwa watumiaji wake ambao ni Wizara, Taasisi na Idara zinazojitegemea.

Alisema kuwa kutokana na maboresho hayo, Wizara ya Fedha inatoa mafunzo ya matumizi ya mfumo huo pamoja na kuelekeza nyaraka zote muhimu zinazohitajika katika uchambuzi wa maombi ya fedha.

“Lengo la kikao kazi hiki ni kutoa mafunzo ya mfumo ulioboreshwa na kujadili mafanikio na changamoto mbalimbali zinazojitokeza wakati wa kutumia mfumo huu kwa ajili ya kuuboresha”, alisema Bw. Kuchaka.

Alifafanua kuwa Matumizi ya mfumo huo yanatokana na Waraka Na. 2 wa Hazina wa Mwaka 2019 kuhusu utaratibu wa kuomba na kuhamisha fedha kutoka kwa Washirika wa Maendeleo kwenda moja kwa moja kwenye miradi ya maendeleo (Direct to Project Funds).

Aidha, Waraka huo umeelekeza Maafisa Masuuli wote Tanzania Bara kuomba kibali kwa Mlipaji Mkuu wa Serikali (Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha), kabla ya kutumia fedha za Washirika wa Maendeleo au kuzihamisha kutoka Benki Kuu kwenda benki za biashara.

No comments:

Post a Comment