Muonekano wa majengo ya miundo mbinu bora ya elimu yaliyojengwa kwa fedha za CSR kutoka mgodi wa Barrick Bulyanhulu katika shule mbalimbali za msingi na sekondari zilizopo wilayani Nyang'hwale na Msalala.
Muonekano wa majengo ya miundo mbinu bora ya elimu yaliyojengwa kwa fedha za CSR kutoka mgodi wa Barrick Bulyanhulu katika shule mbalimbali za msingi na sekondari zilizopo wilayani Nyang'hwale na Msalala.
Wanafunzi wakifuatilia masomo katika miundombinu bora iliyojengwa kupitia miradi ya fedha za CSR za mgodi wa Barrick Bulyanhulu.
Baadhi ya wanafunzi wakiwa katika picha ya pamoja nje ya madarasa ya kisasa wanayosomea ambayo yamejengwa kupitia miradi ya CSR ya mgodi wa Barrick Bulyanhulu.
***
Mgodi wa Barrick Bulyanhulu uliopo katika halmashauri ya wilayani Msalala, Mkoani Shinyanga, umeendelea kuleta mafanikio makubwa kwa wananchi kutokana na kuwa kinara wa kutekeleza sera ya Uwajibikaji kwa Jamii (CSR). Utekelezaji wa sera hiyo umefanikisha miradi mikubwa ya maendeleo ambayo imeboresha maisha ya wananchi wengi wanaoishi maeneo yanayozunguka mgodi huo.
Miradi hiyo inatekelezwa kwa fedha za Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) zinazotolewa na Mgodi huo. Utekelezaji unafanywa kwa kushirikiana na Serikali na Wananchi wenyewe kupitia kamati zao za Maendeleo ambazo huibua miradi kutokana na mahitaji yao. Miradi mikubwa iliyotekelezwa na inayoendelea kutekelezwa ipo kwenye sekta za elimu, afya, Maji, uwezeshaji wa wananchi kiuchumi na ujenzi wa miundo mbinu ya barabara.
Kutokana na umahiri wa kutekeleza miradi ya kijamii (CSR) kwa ufanisi mkubwa hivi karibuni mgodi wa Barrick Bulyanhulu ulitunukiwa tuzo kubwa katika kipengele hicho na Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi katika hafla iliyofanyika mjini Singida.
Miradi iliyotekelezwa
Meneja Mahusiano ya Jamii na Mazingira wa Barrick Bulyanhulu, Bw. Paul Agapiti, aliitaja miradi iliyofanikishwa na Mgodi huo hivi karibuni katika halmashauri za wilaya za Msalala, Kahama na Nyang’wale Mkoani Geita. Katika mkoa huo, Mgodi umejenga Chuo cha Uuguzi Ntobo uliogharimu shilingi milioni 400 pamoja na upanuzi wa kituo cha afya Bugarama chenye uwezo wa kuhudumia wananchi 50,000 kwa mwaka. Mgodi pia umejenga zahanati 28 katika halmashauri za wilaya ya Msalala na Nyang’hwale.
Muonekano wa majengo ya miundo mbinu bora ya elimu yaliyojengwa kwa fedha za CSR kutoka mgodi wa Barrick Bulyanhulu katika shule mbalimbali za msingi na sekondari zilizopo wilayani Nyang'hwale na Msalala.
Miradi mingine ambayo imekamilika na ile inayoendelea kutekelezwa na Mgodi ni ujenzi wa Chuo Cha Ufundi (Bugarama Vocational Education Training Authority-VETA) unaogharimu shilingi milioni 292.5, na ujenzi wa Shule ya Sekondari ya wasichana Bulyanhulu uliogharimu shilingi milioni 822.
Bw. Agapiti, alitaja miradi mingine ambayo ni ujenzi wa Shule ya Msingi ya mchepuo wa kingereza (Nyang’wale English Medium Primary School) uliogharimu shilingi milioni 300, ujenzi wa stendi za mabasi katika mji mdogo wa Segese uliogharimu shilingi milioni 250, ujenzi wa stendi ya kuegesha malori ya Isaka uliogharimu shilingi milioni 485, na mradi wa kusambaza mabomba ya maji yenye urefu wa kilometa 55.7 utakaonufaisha zaidi ya wananchi 100,000 ukiwa umegharimu shilingi Bilioni 4 utakapokamilika.
Baadhi ya wanafunzi wakiwa katika picha ya pamoja nje ya madarasa ya kisasa wanayosomea ambayo yamejengwa kupitia miradi ya CSR ya mgodi wa Barrick Bulyanhulu.
Aidha Bwana Agapiti alisema mgodi wa Bulyanhulu pia umetoa fedha kiasi cha dola za kimarekani milioni 40. Kiasi hicho ni sawa na sawa na zaidi ya shilingi Bilioni 100 za fedha za kitanzania kwa ajili ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kutoka Kahama hadi Kakola ulipo mgodi. Ujenzi wa barabara utarahisisha usafiri na kuchangia katika kukuza uchumi wa eneo hilo. Barabara hiyo itaongeza ufanisi wa usafirishaji wa bidhaa na huduma, na kuchochea maendeleo ya biashara, uwekezaji na kukuza ukuaji wa uchumi katika Mikoa ya Shinyanga na Geita.
Pia upo mradi mkubwa wa kusambaza umeme katika miji ya Kakola, Bugarama na Ilogi uliogharimu dola za kimarekani Milioni 5. Kiasi hicho ni sawa na zaidi ya shilingi Bilioni 13 za fedha za kitanzania. Mgodi huo umejenga madarasa 87. Kati ya hayo madarasa 55 yapo katika Halmashauri ya Msalala na madarasa 32 katika Halmashauri ya Nyang’wale.
Serikali yapongeza ufanikishaji wa miradi hii mikubwa
Akiongea wakati wa ziara ya Wabunge wa kamati ya Afya na Ukimwi Mgodini hapo hivi karibuni, Naibu Waziri wa Madini, Dk. Steven Kiruswa, alisema kampuni ya Barrick si tu moja wa vinara katika sekta ya uchimbaji wa madini bali pia inatekeleza kwa vitendo dhana ya Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) kupitia migodi yake. Alisema jambo hilo limeleta mabadiliko makubwa Kwa wananchi wanaoishi karibu na migodi hiyo hususani katika sekta za elimu, afya, maji, miundombinu ya barabara, pamoja na ufundi stadi.
Wadau waongea kuhusu athari chanya za miradi ya CSR ya Barrick Bulyanhulu
Wananchi wanaoishi katika maeneo ya miradi katika halmashauri za Wilaya za Nyang’hwale, Msalala, wameshukuru Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa kufanikisha miradi miradi mikubwa kupitia fedha za CSR. Miradi hiyo ambayo inaendelea kuyafanya maisha yao kuwa bora itadumu kwa muda mrefu, pia itanufaisha vizazi vijavyo hata baada ya kufungwa kwa shughuli za mgodi.
Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Buyange wakifuatilia masomo katika miundombinu bora iliyojengwa kupitia miradi ya fedha za CSR za mgodi wa Barrick Bulyanhulu.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Bugarama Evelyn Kajigili anasema “Miradi ya CSR ya Barrick Bulyanhulu kwa kushirikiana na Serikali imeleta faraja kubwa kwa wanafunzi kwa sababu kuboresha mazingira ya kusomea, kuimarisha usalama wa watoto wa kike kutokana na kujengewa mabweni ya kisasa, hali ambayo inachangia kuongezeka kwa kiwango cha ufaulu wa wanafunzi, kupunguza utoro na kukomesha mimba za utotoni”.
Mwalimu Lucia Anatory wa Shule ya Mchepuo wa Kiingereza ya Karumwa iliyopo Halmashauri ya Nyang’hwale alisema mradi wa Barrick Bulyanhulu wa ujenzi wa shule hiyo umewezesha watumishi na wafanyabiashara waliokuwa wanawapeleka watoto wao kusoma mbali kuondokana na adha hiyo.
Wanafunzi wakifuatilia masomo katika miundombinu bora iliyojengwa kupitia miradi ya fedha za CSR za mgodi wa Barrick Bulyanhulu.
Alisema jambo la kufurahisha kupitia fedha za CSR za Barrick Bulyanhulu, shule nyinginezo za Serikali zimeendelea kuimarishwa kwa miundombinu kwa kujengewa maabara za kisasa, mabweni, majiko na, kununuliwa madawati. Mwalimu Lucia alisema kuboreshwa kwa miundombinu kumewawezesha watoto kupata elimu katika mazingira rafiki.
Miradi ya Uwezeshaji Jamii
Kwa upande wa miradi ya uwezeshaji jamii, Mgodi wa Barrick Bulyanhulu umeendelea kufadhili miradi mbalimbali ambayo inawanufaisha wananchi moja kwa moja. Miradi hiyo ni pamoja na ufugaji wa nyuki, na kutoa mafunzo maalum ya ujasiriamali kwa wananchi hususani Wanawake na vijana.
Belitha Nyawanga, Mkazi wa Kijiji cha Buyange ambaye ni miongoni mwa wanufaika wa mradi wa kufuga nyuki alisema kuwa kipato cha familia yake kimeongezeka tangu alipojiunga kwenye kikundi cha kufuga nyuki baada ya mafunzo kutoka kwa wataalamu mwaka 2020.
“Tayari familia yangu imeanza ujenzi wa nyumba bora na kisasa kutokana na kipato kinachotokana na ufugaji wa nyuki na kuna familia nyingi zimenufaika kwa namna tofauti kutokana na uwezeshaji wa mgodi wa Barrick Bulyanhulu,” Belitha alisema.
Agnes Andrew, mama lishe kutoka Kijiji cha Bunango ambacho ni miongoni mwa vijiji vya kata ya Bugarama vinavyonufaika na miradi ya CSR anasema biashara yake imeimarika kwa kasi kutokana na ongezeko la mauzo ya chakula kwa wateja.
Wanafunzi wanena kuhusu Miradi
Angel Taitas ambaye ni Mwanafunzi wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Bugarama ambaye kwa sasa anaishi Katika Bweni lililojengwa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, akiongea kwa niaba ya Wanafunzi wenzake, amesema ndoto zake za kuendelea na masomo zilianza kufifia kutokana na changamoto za mazingira alizozipata wakati akisoma akitokea nyumbani, ila kwa sasa anafurahia mazingira yaliyoboreshwa shuleni hapo.
Aliongeza kwamba sasa ndoto za Wanafunzi wengi zinaenda kutimia kutokana na Shule hiyo kuwa na miundombinu rafiki kwa ajili ya kujifunzia na ameushukuru Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa Kushirikiana na Serikali kwa Kuwaboreshea Miundombinu ya Shule yao.
No comments:
Post a Comment