NACTVET YAFUNGUA RASMI DIRISHA LA UDAHILI WA WANAFUNZI 2025/2026 - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, May 28, 2025

NACTVET YAFUNGUA RASMI DIRISHA LA UDAHILI WA WANAFUNZI 2025/2026



Na Okuly Julius, DODOMA



Serikali kupitia Baraza la Taifa la elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi (NACTVET) limefungua Rasmi dirisha udahili wa wanafunzi kwa mwaka wa masomo 2025/2026 kwa ngazi za Astashahada na Stashahada katika kozi zote zinazosimamiwa baraza hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Dkt Mwajuma Lingwanda amesema udahili wa wanafunzi umefunguliwa Rasmi mei 28 hadi Julia 11 mwaka huu.

Ambapo amesema Muombaji anaweza kuomba Chuo zaidi ya kimoja na kuchaguliwa katika Chuo alichoomba kutategemea ushindani utakao kuwepo katika Chuo hicho.


"Muombaji akishachaguliwa na Chuo, Chuo husika kitawasilisha taarafa za muombaji NACTVET kwa ajili ya uhakika,Muombaji atapokea ujumbe ukimtaarifu kuwa taarifa zake zimewasilishwa NACTVET na Chuo kwa ajili ya kuhakikiwa," amesema Dkt. Lingwanda

Katika hatua Nyingine Dkt Lingwanda ameweka wazi mambo ya kuzingatia kwa waombaji kupitia mfumo wa udahili wa pamoja yaani (Central Admission system - CAS)

Pia Baraza hilo limeendelea limewasisitiza waombaji kuhusika moja kwa moja katika zoezi zima la kuomba kudahiliwa pamoja na kuandika Taarifa zao kwa usahihi na kutunza kumbukumbu.

"Maombi ya kozi zisizo za afya (Tanzania Bara na Zanzibar) kwa kozi zote ambazo si za Afya wala Sayansi Shirikishi, waombaji wanapaswa kuwasilisha maombi yao moja kwa moja kwenye vyuo husika kuanzia 28 Mei hadi 11 Julai 2025,"

Na kuongeza kuwa "Maombi ya kozi za Afya na Sayansi Shirikishi (Tanzania Bara):Maombi yatawasilishwa kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS – Central Admission System) unaopatikana kwenye tovuti ya NACTVET: www.nactvet.go.tz," amesisitiza Dkt. Lingwanda anda

Baraza pia limewashauri waombaji wote kusoma kitabu cha mwongozo wa udahili kwa mwaka 2025/2026 ambacho kinapatikana kwenye tovuti ya Baraza. Kitabu hiki kinaeleza sifa za kujiunga na kozi mbalimbali na orodha ya vyuo vinavyotoa kozi hizo.

No comments:

Post a Comment