Na Okuly Julius _ DODOMA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, amewahimiza Watanzania kuonyesha uzalendo kwa vitendo kwa kujitokeza kwa wingi kujiandikisha na kuboresha taarifa zao katika Daftari la Kudumu la Mpiga Kura, ili waweze kutumia haki yao ya kikatiba ya kupiga kura na kuchagua viongozi wanaoamini watawaletea maendeleo.
Akizungumza leo Mei 17, 2025 katika eneo la Chamwino mkoani Dodoma, muda mfupi baada ya kuboresha taarifa zake na kupata kitambulisho cha mpiga kura, Rais Samia amesema ni wajibu wa kila raia kuhakikisha anashiriki kikamilifu katika mchakato wa uchaguzi kwa kujiandikisha mapema.
“Kila mtu ana haki ya kikatiba ya kupiga kura kuchagua viongozi. Hivyo kutoshiriki katika mchakato wa kujiandikisha au kuhuisha taarifa kwenye Daftari la Kudumu la Mpiga Kura ni sawa na mtu kujinyima haki yake ya kikatiba kwa hiari, jambo ambalo siyo uzalendo,” amesema Dkt. Samia.

Ameongeza kuwa, “Ukikataa kujiandikisha, unakosa nafasi ya kumchagua kiongozi unayemtaka.”
Rais Samia amesema kuwa kutokana na umuhimu wa zoezi hilo, ameamua kushiriki kama mkazi wa Chamwino, ambako pia atapiga kura katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.
Ameeleza kuwa amerekebisha taarifa zake ili kuhakikisha anakuwa tayari kushiriki kikamilifu katika mchakato wa uchaguzi, na amewakumbusha wananchi kuwa huu ni mzunguko wa pili na wa mwisho wa uandikishaji na uhuishaji wa taarifa.
“Baada ya awamu hii, hakutakuwa na nafasi nyingine ya kujiandikisha. Hivyo basi, tumieni fursa hii kwa uzalendo na kwa manufaa yenu wenyewe,” amesisitiza.
Rais Samia pia amewahimiza wananchi kuwa wavumilivu pale changamoto zinapojitokeza katika vituo vya kujiandikisha, huku akibainisha kuwa Serikali imeweka mipango madhubuti kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma stahiki.
“Tuonyeshe uzalendo kwa vitendo. Tujitokeze kwa wingi, tuhimize wengine, na tusisite kufika vituoni,” alihimiza.
Naye Ofisa mwandikishaji wa Majimbo ya Chamwino na Mvumi Godfrey Mnyamale amesema shughuli hiyo inakwenda kuwaandikisha wapiga kura wapya wenye sifa na kuhakiki taarifa ya waliojiandikisha
Zoezi la uandikishaji na uhuishaji linaendelea katika maeneo mbalimbali nchini, ikiwa ni hatua muhimu kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

No comments:
Post a Comment