REB WASISITIZA WAKANDARASI KUKAMILISHA MIRADI UMEME VIJIJINI KWA WAKATI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, May 15, 2025

REB WASISITIZA WAKANDARASI KUKAMILISHA MIRADI UMEME VIJIJINI KWA WAKATI


Wajumbe wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB) wametoa wito kwa Wakandarasi wanaojenga Miradi ya umeme vijijini katika mkoa wa Kilimanjaro husasan wilaya ya Mwanga, Same na Hai mkoani humo kufanya kazi kwa haraka ili kukamilisha Miradi ya usambazaji wa nishati ya umeme mkoani humo.

Wito huo, umetolewa Wajumbe wa Bodi kwenda kwa Wakandarasi (Kampuni ya Northern Engineering Works Ltd; RADI Service Ltd; Transpower Limited pamoja na Kampuni ya Octopus Engineering Ltd. Wakandarasi wote hao wanaendelea na utekelezaji Miradi hiyo katika hatua mbalimbali huku ikielezwa kuwa shilingi bilioni 14 zilitengwa kwa ajili ya kugharamia Miradi hiyo.

“Natoa wito wa kufanya kazi kwa juhudi na weledi ili kukamilisha Miradi ya kusambaza nishati ya umeme vijijini kwa kuwa Serikali inatumia fedha nyingi ili licha ya kuwa Wakandarasi wengi katika mkoa wa Kilimanjaro wanafanya kazi vizuri, tufanye kazi kwa kasi na tusitumie kisingio chochote hata kama ni changamoto ya hali ya hewa, ni vizuri tuzingatie ukomo wa muda (Deadline)”, amesema Mhe. Barozi, Radhia Msuya.

Kwa upande wa Miradi ya kusambaza umeme kwenye vitongoji; REB imetoa wito pia kwa Mkandarasi (Kampuni ya Ceylex Engineering [Pvt] Ltd) kuendelea na kasi ya kusambaza umeme kwenye vitongoji 134 licha ya changamoto hali ya hewa ya mvua na jiographia.

Mkoa wa Kilimanjaro una jumla ya vitongoji 2,260 ambapo vitongoji 1,974 sawa na asilimia 87.34% vimeshafikiwa na huduma ya umeme kupitia miradi ya REA iliyopita na inayoendelea mkoani Kilimanjaro na kufanya idadi ya vitongoji 286 pekee kusalia pasipokuwa na huduma ya umeme.

Miongoni mwa vitongoji hivyo, vitongoji 94 sambamba na vitongoji vingine 41 vinavyofanya jumla ya vitongoji 135 vipo katika mradi huu wa kupeleka umeme katika vitongoji vyote nchini Awamu ya Pili A; Fungu la 08.

Akitoa taarifa mbele ya Wajumbe wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB); Mhandisi Miradi ya REA mkoa wa Kilimanjaro, Mhandisi Kelvin Melchiad amesema Mradi huo wa vitongoji unalenga kupeleka umeme katika vitongoji 135 vya mkoa wa Kilimanjaro.

“Mradi huu wa (HEP 2) unalenga kusambaza umeme kwenye vitongoji ambavyo havijafikiwa na umeme ikiwa na maana vitongoji 15 kwa kila jimbo katika majimbo yote 9 ya Mkoa wa Kilimanjaro,kazi inayotekelezwa na Mkandarasi Ceylex Engineering (Pvt) Ltd kwa gharama ya shilingi bilioni 18; Mradi unaofadhiliwa na Serikali ya Tanzania kwa asilimi 100.
Mradi unatarajiwa kukamilika ndani ya kipindi kisichozidi siku 730 tangu kuanza kwake tarehe 03 Septemba, 2024 na utakamilika tarehe 03 Septemba, 2026, na utajenga wigo wa msongo mdogo wa umeme (LV Line) wa kilomita 270, Mashine Umba 135 zenye ukubwa wa 100 kVA na kuunganisha jumla ya wateja 4,455 kwa mkoa wote wa Kilimanjaro.

Katika hatua nyingine Wajumbe Bodi ya Nishati Vijijini wametoa wito kwa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mkoani Kilimanjaro kuongeza wigo wa sharti la vitambulisho vingine kama Kitambulisho cha Mpiga Kura ili kuwezesha kusajiri Wananchi ili waunganishwe na huduma ya umeme majumbani mwao badala ya sasa ambapo kinatumika Kitambulisho cha NIDA pekee; hali hiyo inachangia Wananchi wengi wa vijijini kukosa sifa ya kuunganishwa na huduma hiyo kwa kuwa wengi wao hawana Vitambulisho hivyo.

Wakati huo huo; Wajumbe wa Bodi ya Nishati Vijijini walipata pia nafasi ya kutembelea Gereza la wilaya ya Mwanga na kujionea namna Jeshi la Magereza linavyotekeleza kwa vitendo matumizi ya Nishati Safi kwa kupika vyakula vya Wafungwa wapatao 74 katika gereza hilo; walipata nafasi pia ya kula chakula cha mchana kilichoandaliwa kwa ajili ya Wafungwa kwa kutumia teknolojia ya Nishati Safi ya Kupikia kwenye Gereza hilo.

No comments:

Post a Comment