Na Okuly Julius DODOMA
Wizara ya Uchukuzi imesema katika mwaka wa fedha 2025/26, jumla ya Shilingi milioni 833.22 fedha za nje zimetengwa kwa ajili ya kutekeleza Mradi wa Uboreshaji wa Usalama wa Usafiri na Usafirishaji katika Bahari na Maziwa Makuu.
Hayo yameelezwa na Waziri wa Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa leo Bungeni Jijini Dodoma wakati akitoa hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Uchukuzi kwa mwaka wa fedha 2025/2026.
Amesema Fedha hizo zitatumika katika kukamilisha ujenzi wa Kituo Kikuu cha Uratibu wa Utafutaji na Uokoaji (MRCC) katika Ziwa Victoria,kukamilisha ujenzi wa vituo vitatu (3) vya utafutaji na uokoaji katika maeneo ya Nansio – Ukerewe, Musoma Mjini, na Kanyala – Sengerema katika Ziwa Victoria;
iii. Kukamilisha ununuzi wa boti ya huduma ya dharura (Ambulance Boat) kwa ajili ya kutoa huduma katika Ziwa Victoria.
Amesema mambo miradi mingine itakayotekelezwa katika eneo la Bahari na Maziwa makuu ni kukamilisha ununuzi wa boti mbili (2) za utafutaji na uokoaji katika Ziwa Victoria ,kufanya Upembuzi Yakinifu wa kuboresha shughuli za utafutaji na uokoaji katika Ziwa Tanganyika na Ziwa Nyasa.
"Kufanya Upembuzi Yakinifu na Usanifu wa kina kwa ajili ya kuhuisha ramani za urambazaji,kuweka alama za kuongoza meli katika Maziwa Makuu na Kuratibu Sensa ya kuhuisha kanzidata ya vyombo vidogo vya usafiri majini; na Kuunda mfumo wa TEHAMA wa ufuatiliaji na usimamizi wa vyombo vya usafiri majini,"ameanisha Profesa Mbarawa
No comments:
Post a Comment