Na WAF, DODOMA
Serikali kupitia Wizara ya Afya imetenga Shilingi Bilioni 123.9 kwa mwaka wa fedha 2025/26 kwa ajili kuimarisha huduma za matibabu ya ubingwa na ubingwa bobezi pamoja na kuimarisha tiba utalii nchini.
Hayo yamebainishwa na Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama Juni 02, 2025 Bungeni jijini Dodoma, wakati akiwasilisha Bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2025/26 ambapo fedha hizo ni kwa ajili ya kuendelea kutoa huduma za matibabu ya ubingwa na ubingwa bobezi katika Hospitali ya Taifa, Hospitali maalum, Hospitali za Rufaa za Kanda na Hospitali za Rufaa za Mikoa pamoja na kuanzisha na kuimarisha huduma mpya kulingana na mahitaji ya sasa.
Amesema upandikizaji wa ini katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kuanzisha huduma bobezi za mfumo wa mkojo na uzazi kwa wanaume (Uro-andrology) katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kampasi ya Mloganzila ni sehemu ya kipaumbele katika kutangaza tiba utalii.
No comments:
Post a Comment