
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, akikabidhiwa Jarida la ‘’Hazina Yetu’’ Toleo la Tatu kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025, na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha, Bw. Benny Mwaipaja, ofisini kwake, Treasury Square, jijini Dodoma, ambapo amekipongeza Kitengo hicho kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kutangaza na kuhabarisha umma kuhusu Sera, Program, Mikakati na Mipango mbalimbali inayofanywa na Wizara katika kusimamia uchumi wa nchi.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El- maamry Mwamba akipitia kurasa za Jarida la ‘’Hazina Yetu’’ Toleo la Tatu kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025, baada ya Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha, Bw. Benny Mwaipaja, kumkabidhi nakala ya Jarida hilo, ofisini kwake, Treasury Square, jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El- maamry Mwamba akionesha Jarida la ‘’Hazina Yetu’’ Toleo la Tatu kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025, baada ya Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Bw. Benny Mwaipaja, kuwakabidhi ofisini kwa Katibu Mkuu, Treasury Square, jijini Dodoma,

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watumishi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha, wakionesha Jarida la ‘Hazina Yetu’ Toleo la Tatu kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025, baada ya Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha, Bw. Benny Mwaipaja, kumkabidhi Katibu Mkuu, ofisini kwake, Treasury Square, jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Natu El- maamry Mwamba, akizungumza na Watumishi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, wakati walipofika ofisini kwake kwa ajili ya kumkabidhi Jarida la ‘Hazina Yetu’, Toleo la Tatu kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025, Treasury Square, jijini Dodoma, ambapo amekipongeza Kitengo hicho kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kutangaza na kuhabarisha umma kuhusu Sera, Program, Mikakati na Mipango mbalimbali inayofanywa na Wizara katika kusimamia uchumi wa nchi.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha, Bw. Benny Mwaipaja, akizungumza wakati alipowasili pamoja na Watumishi wa Kitengo chake kwa ajili ya kumkabidhi Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Jarida la ‘’Hazina Yetu’’ Toleo la Tatu kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025, ofisini kwake, Treasury Square, jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba akioneshwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha, Bw. Benny Mwaipaja, baadhi ya makala, matukio na picha zilizopo katika, Jarida la ‘’Hazina Yetu’’ Toleo la Tatu kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025 baada ya kukabidhiwa jarida hilo, ofisini kwake, Treasury Square, jijini Dodoma.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dodoma)
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu Elmaamry Mwamba, amepokea Jarida la Hazina Yetu Toleo la Tatu kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025 linaloandaliwa na Wizara kupitia Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kila baada ya miezi mitatu.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa Jarida hilo na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha, Bw. Benny Mwaipaja, Katibu Mkuu, Dkt. Mwamba, alipongeza kazi kubwa na nzuri inayofanywa na Kitengo hicho katika kuhabarisha umma kuhusu Sera, Program, Mikakati na Mipango mbalimbali inayofanywa na Wizara katika kusimamia uchumi wa nchi na kwa kuandaa Jarida hilo katika viwango vya hali ya juu.
Aliahidi kuwa Wizara itaendelea kikiwezesha Kitengo hicho ili kiongeze vifaa vya kisasa vya kukusanya, kuchakata na kusambaza habari kwa wadau mbalimbali wa wizara walioko ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.
Jarida la “Hazina yetu”limesheheni maarifa mbalimbali kupitia makala, habari, matukio, habari picha na matangazo mbalimbali na husambazwa kwa njia ya nakala ngumu (hard copies) na nakala tete (soft copies) kupitia mitandao ya kijamii ya Wizara na wadau wengine wa habari pamoja na Tovuti ya Wizara ya Fedha www.mof.go.tz
No comments:
Post a Comment