Na.Mwanadishi Wetu - Dodoma
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mwakilishi wa Shirika la World Vision Tanzania Dkt. Joseph Mayala leo tarehe 24 Juni, 2025 Jijini Dodoma.
Lengo la kikao hicho ni shirika hilo kujitambulisha lakini pia kushukuru kwa ushirikiano uliopo kati ya Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu pamoja na shirika hilo hasa katika masuala ya Lishe na yanayohusu menejimenti ya maafa nchini.
Aidha, Dkt. Yonazi ameahidi kuzidi kushirikiana na shirika hilo hasa katika maeneo ya lishe na masuala ya maafa ili kuhakikisha huduma za serikali zinawafikia wananchi.
Dkt. Yonazi aliwahakikishia wadau hao kuendeleza ushirikiano kwa kutambua mchango wao wa hali na mali kila ilipohitajika akitolea mfano Maafa mbalimbali yaliyowahi kuikumba nchi ya Tanzania.
"Nawapongeza World Vision mmeendelea kutukimbilia kila inapobidi hususan nyakati za maafa yanapotokea, hili limekuwa jambo nzuri la kuigwa, asanteni na tutaendelea kushirikiana nanyi” alisema Dkt. Yonazi
No comments:
Post a Comment