MSD YAPELEKA JOKOFU LA KUHIFADHI MIILI KITUO CHA AFYA MUGETA, BUNDA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, June 10, 2025

MSD YAPELEKA JOKOFU LA KUHIFADHI MIILI KITUO CHA AFYA MUGETA, BUNDA


Na, WAF-Dodoma


Serikali kupitia Bohari Kuu ya Dawa (MSD) imethibitisha kuwa tayari imepeleka jokofu moja la kuhifadhi miili lenye uwezo wa kuhifadhi miili sita (6) katika Kituo cha Afya Mugeta, wilaya Bunda, mkoani Mara.

Akijibu swali la Mbunge wa Bunda, Mhe. Boniphace Mwita Getere, leo Juni 10, 2025 Bungeni jijini Dodoma aliyetaka kujua ni kwa nini tangu mwaka 2018 hadi sasa MSD haijapeleka majokofu manne (4) ya mochwari katika kituo hicho, Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel, amesema jokofu hilo lilifikishwa katika kituo hicho Februari 21, 2024 na linaendelea kufanya kazi vizuri.

“Serikali itaendelea kununua na kusambaza vifaa tiba katika vituo vya kutolea huduma za afya kulingana na upatikanaji wa fedha,” amesema Dkt. Mollel.

Aidha, Dkt. Mollel amebainisha kuwa Serikali imetenga zaidi ya shilingi milioni 980 kwa ajili ya kuboresha na kukamilisha ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Bunda, hatua inayolenga kuongeza upatikanaji wa huduma bora za afya kwa wakazi wa wilaya hiyo.

Katika kuimarisha upatikanaji wa dawa na vifaa tiba nchini, Dkt. Mollel ameongeza kuwa MSD tayari imepokea zaidi ya shilingi bilioni 100 kama mtaji wa kuimarisha uwezo wake wa kifedha. Mtaji huo unalenga kuiwezesha MSD kushirikiana na wadau mbalimbali wa sekta ya afya katika kuongeza uzalishaji wa dawa na kuimarisha upatikanaji wake nchini kote.

No comments:

Post a Comment