
Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu,akipata maelezo kutoka kwa Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa EWURA ,Tobietha Makafu,mara baada ya kutembelea Banda la EWURA,katika maonesho ya wiki ya Utumishi wa umma yanayoendelea katika viwanja vya Chinangali jijini Dodoma.
Na Alex Sonna, Dodoma
Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,Mhe. Deus Sangu, amesema Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) ni miongoni mwa taasisi za umma zilizofanikiwa kuonesha matokeo ya utumishi wenye tija kwa wananchi kupitia usimamizi makini wa huduma muhimu nchini.
Mhe.Sangu ameyasema hayo leo Juni 20,2025 mara baada ya kutembelea banda la EWURA kwenye maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea jijini Dodoma.
Ameeleza kuwa EWURA imefanya kazi kubwa kupambana na changamoto zilizokuwa zikiwasumbua Watanzania, hasa tatizo la uchakachuaji wa mafuta ambalo sasa limebaki historia.
“Nawapongeza kwa dhati kwa kazi mnayofanya,zamani wananchi walilalamikia mafuta feki kila kona, lakini leo hatusikii tena tatizo hilo,huu ni ushahidi kuwa EWURA inatekeleza wajibu wake kwa umahiri mkubwa,” amesema Mhe. Sangu.
Aidha ameongeza kuwa EWURA inalo jukumu kubwa la kuendeleza jitihada hizo kwa kuhakikisha walaji wanalindwa zaidi, huku wazawa wakipewa nafasi katika miradi ya sekta ya nishati na maji kupitia usimamizi thabiti wa maudhui ya ndani, ili kuhakikisha Watanzania wananufaika na rasilimali za nchi yao.
Mhe.Sangu amehitimisha kwa kusisitiza kuwa mfano uliowekwa na EWURA unapaswa kuigwa na taasisi nyingine za umma kwa kuwa ni kielelezo cha utumishi wenye ufanisi, uwajibikaji na unaoweka mbele maslahi ya wananchi.
Naye Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa EWURA ,Tobietha Makafu,ameeleza kuwa maonesho hayo yamekuwa fursa ya kusikiliza maoni ya wananchi, kutoa elimu kuhusu haki na wajibu wa watumiaji wa huduma, na kujenga uhusiano wa moja kwa moja kati ya taasisi hiyo na jamii.

Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu,akipata maelezo kutoka kwa Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa EWURA ,Tobietha Makafu,mara baada ya kutembelea Banda la EWURA,katika maonesho ya wiki ya Utumishi wa umma yanayoendelea katika viwanja vya Chinangali jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu,akitoa maoni kuhusu shughuli za udhibiti wa huduma za nishati na maji, alipotembelea banda la EWURA, katika maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika viwanja vya Chinangali,jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu,akipokea zawadi kutoka kwa Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa EWURA ,Tobietha Makafu,mara baada ya kutembelea Banda la EWURA,katika maonesho ya wiki ya Utumishi wa umma yanayoendelea katika viwanja vya Chinangali jijini Dodoma.
No comments:
Post a Comment