RAIS SAMIA ATANGAZA JINA JIPYA LA BARABARA YA MZUNGUKO WA NJE DODOMA KUWA "BARABARA YA AKINWUMI ADESINA" - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, June 14, 2025

RAIS SAMIA ATANGAZA JINA JIPYA LA BARABARA YA MZUNGUKO WA NJE DODOMA KUWA "BARABARA YA AKINWUMI ADESINA"




Na Okuly Julius_ DODOMA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametangaza rasmi jina jipya la Barabara ya Mzunguko wa Nje wa Jiji la Dodoma yenye urefu wa kilomita 112.3 kuwa "Barabara ya Akinwumi Adesina."

Akizungumza katika eneo la Nala, mkoani Dodoma, mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara hiyo pamoja na ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato, Rais Samia amesema amekubali ombi la Waziri wa Ujenzi, Mhe. Abdallah Ulega, la kuipa barabara hiyo jina hilo, ikiwa ni ishara ya kutambua mchango mkubwa wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) katika sekta ya miundombinu nchini.

"Kwa kutambua juhudi na mchango mkubwa wa AfDB chini ya uongozi wa Rais wake, Dkt. Akinwumi Adesina, katika kuunga mkono miradi ya maendeleo hapa nchini, ikiwemo ujenzi wa barabara hii muhimu, nimeridhia ombi la kuitwa Barabara ya Akinwumi Adesina," alisema Rais Samia.

Barabara ya Mzunguko wa Nje wa Jiji la Dodoma ni miongoni mwa miradi mikubwa ya kimkakati inayotekelezwa kwa ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na wadau wa maendeleo, ikiwemo AfDB, kwa lengo la kuboresha mtandao wa usafiri na kuchochea ukuaji wa uchumi katika mkoa huo mkuu wa nchi.





No comments:

Post a Comment