TOVUTI YA NANE NANE 2025 YAZINDULIWA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, June 14, 2025

TOVUTI YA NANE NANE 2025 YAZINDULIWA


Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe (Mb) amezindua Tovuti ya Usajili kwa ajili ya Ushiriki wa Maonesho ya Nane Nane 2025 yatakayofanyika Kitaifa Mkoani Dodoma tarehe 1 hadi 8 Agosti 2025.

Mkutano huo na Wanahabari umefanyika tarehe 13 Juni 2025, jijini Dodoma na kuhudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Bw. Gerald Mweli.

Usajili huo utaanza tarehe 17 Juni 2025 hadi 16 Julai 2025 ambapo Waziri Bashe amesisitiza Taasisi na Mashirika ya Umma kujisajili kwa wakati katika tovuti hiyo.

Kauli mbiu ni "Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo Mifugo na Uvuvi 2025", ambapo Waziri Bashe ameeleza kuwa ujenzi wa uwanja wa Nane Nane Dodoma unaendelea ukitarajiwa kuwa na kituo cha kitaifa cha zana za kilimo pamoja na kituo na uunganishi wa ndege nyuki za kilimo (drone assembly hub) katika kumuwezesha mkulima kuzifikia zana za kilimo kwa ajili ya uzalishaji.

Aidha, Waziri Bashe amesema kuwa kuna maboresho makubwa yamefanyika kwenye uwanja wa Nzuguni Dodoma ikiwemo kuongeza maeneo ya huduma za kijamii kama vile maeneo ya wajasiriamali nakadhalika ambavyo vitasaidia watu kufanya shughuli zao.

Ameongeza kuwa vipando vimeendelea kupandwa kuelekea maonesho hayo na kusema ili kurahisisha shughuli za kilimo, visima vya kutosha vimechimbwa ili kuwawezesha wakulima kufanya shughuli zao kwenye uwanja huo.





No comments:

Post a Comment