
SHIRIKA la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limesema linaendelea kufanya ukaguzi wa vyombo vya usafiri majini ili kuhakikisha usalama wa abiria na mizigo wanapotumia usafiri huo.
Akizungumza alipotembelea banda la TASAC katika maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene alipongeza Shirika hilo kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kudhibiti vyombo vya usafiri majini.
“Niwapongeze kwa kazi kubwa mnayofanya katika kuhakikisha vyombo vya majini vinafanya shughuli zake kwa usalama wa hali ya juu,” alisema

Kwa upande wake Afisa Msajili na Mkaguzi wa Vyombo vya Usafiri Majini Mkuu TASAC, Mhandisi Saidi Mkwawa alisema Shirika hilo litaendelea kufanya ukaguzi wa mara kwa mara ili kuhakikisha vyombo hivyo vinatoa huduma bora na salama.
“Tunaposema tunadhibiti maana yake tunawapa ushauri wanaotengeza boti, meli kubwa na ndogo kutengeneza kwa viwango vinavyohitajika.
Aliongeza kuwa,”tumekuwa tukifanya ufuatiliaji wa karibu kwa watoa huduma hawa ili kuhakikisha huduma inayotolewa ni ya viwango vya kimataifa ili kuwa na usafiri bora, salama na wa uhakika.
Naye Afisa Uhusiano Mwandamizi wa TASAC Bi. Amina Miruko, alisema Shirika hilo limeanzishwa kwa mujibu wa sheria ya uwakala wa meli sura ya 415 na kuanza kutekeleza majukumu yake rasmi mwaka 2018.
“Majukumu ya Shirika ni kusimamia na kudhibiti sekta ya usafiri wa majini kuwezesha biashara ya usafirishaji majini na kufanya biashara ya uwakala wa meli.

No comments:
Post a Comment