Liverpool inajiandaa kuwasilisha ombi rasmi la kumsajili beki wa Bournemouth na Hungary Milos Kerkez, 21, ambaye tayari amekubali uhamisho huo na thamani yake inakadiriwa na The Cherries kuwa zaidi ya £40m. (GiveMeSport)
Juhudi za Liverpool kumsajili mchezaji wa Bayer Leverkusen Mjerumani Florian Wirtz, 22, zimegonga mwamba. Klubu hiyo sasa huenda ikalazimika kuwatoa wachezaji wa England wa chini ya miaka 21 Harvey Elliott, 22, na Jarell Quansah, 22, kama sehemu ya makubaliano ya kubadilishana wachezaji. (Kicker via Mirror)
Mshambuliaji wa Ipswich na England wa chini ya umri wa miaka 21 Liam Delap, 22, amekamilisha sehemu ya kwanza ya vipimo vyake vya afya kwa ajili ya uhamisho wa pauni milioni 30 kuelekea Chelsea. (Fabrizio Romano)
Everton inavutiwa na kiungo wa Brighton Matt O'Riley, 24, lakini haina uhakika kama Seagulls itamuuza mchezaji huyo wa kimataifa wa Denmark (Sky Sports)
Mkufunzi wa zamani wa Napoli, Chelsea na Juventus Maurizio Sarri, 66, anakaribia kurejea kwa mara ya pili kama kocha mkuu wa Lazio. (Fabrizio Romano)
Bayer Leverkusen imekubali ada ya thamani ya euro 10m (£8.43m) kumsajili kipa wa Uholanzi Mark Flekken mwenye umri wa miaka 31 kutoka Brentford. (Sky Germany)
Brentford imefikia mkataba wa awali wa pauni milioni 12.5, utakaoongezeka hadi pauni milioni 18, na Liverpool kumsajili kipa wa Jamhuri ya Ireland Caoimhin Kelleher, 26, kuchukua nafasi ya Flekken. (Sky Sports)
Kocha wa Inter Milan Simone Inzaghi, 49, atafanya uamuzi ifikapo Jumatano iwapo atakubali ofa ya kuwa kocha wa Al-Hilal ili kuinoa timu hiyo ya Ligi ya Saudi Pro kwenye Kombe la Dunia la Vilabu la Fifa mwezi huu. (Rudy Galetti)
Mkurugenzi wa michezo wa Barcelona Deco amesema hana mpango wa kumtafuta mshambuliaji mpya baada ya klabu hiyo kuhusishwa na mshambuliaji wa Sporting wa Sweden Viktor Gyokeres, 26, ambaye pia ananyatiwa na Arsenal na Manchester United. (A Bola via Mirror)
Kipa wa Ujerumani Marc-Andre Ter Stegen, 33, anasema "hana wasiwasi" kuhusu nafasi yake Barcelona, ambayo inahusishwa na mlinda lango wa Espanyol Joan Garcia, 24. (Forbes).
No comments:
Post a Comment