
Mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma Tanzania kwa Shule za Msingi na Sekondari Nchini, yanahitimisha rasmi leo juni 29,2025 Mkoani Iringa.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI anayeshughulikia Afya, Dkt.Festo Dugange anaongoza sherehe hizo za ufungaji katika viwanja vya Shule ya Sekondari Lugalo Manispaa ya Iringa.
Mashindano ya UMITASHUMTA & UMISSETA 2025, yalifunguliwa rasmi na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa Juni 09,2025.
Ofisi ya Rais-TAMISEMI ndiyo iliyoandaa Mashindano hayo,ikishirikiana na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia pamoja na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.










No comments:
Post a Comment