
WAKILI Eric Kidyalla ni moja ya makada waliojitokeza kuchukua fomu ya kuwania kugombea ya Ubunge kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia Jimbo la Dodoma Mjini.
Alisema sababu iliyomsukuma kuchukua fomu hiyo ni kwa kuwa yeye ni kada wa Chama hicho hivyo aliona ni vyema kutumia haki yake ya kikatiba ili akifanikiwa aweze kutoa mchango wake katika kulitumikia Chama na wanaDodoma mjini akishirikiana na watendaji wengine.
Pia ampongeza Rais, Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia Jimbo la Dodoma mjini liweza kugawanyika jambo ambalo limetoka fulsa kubwa kwa wanaCCM wengi kujitokeza kugombea.
"Jimbo la Dodoma mjini kijiografia lilikuwa kubwa hivyo kuridhiwa ligawanywe, Rais, Samia amefanya jambo jema na itatoanfulsa kubwa kwa wananchi,"alisema Kidyalla



No comments:
Post a Comment