WANANCHI WANUFAIKA NA ELIMU YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA KATIKA MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, June 18, 2025

WANANCHI WANUFAIKA NA ELIMU YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA KATIKA MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA


Wakala wa Nishati Vijijini (REA), leo Juni 18 umeendelea kutoa elimu kuhusu nishati safi ya kupikia kwa wananchi waliotembelea banda la Wakala huo katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika viwanja vya Chinangali Jijini Dodoma.

Maadhimisho hayo ambayo yanatarajiwa kuhitimishwa Juni 23 yameanza Juni 16 yakiwa na kauli mbiu inayosema “Himiza Matumizi ya Mifumo ya Kidijiti ili Kuongeza Upatikanaji wa Taarifa na Kuchagiza Uwajibikaji”.

Wananchi wa rika zote kutoka Mkoani Dodoma na Mikoa ya karibu wameonekana kuvutiwa na banda la REA ambapo wataalam kutoka REA wamewapa taarifa kuhusu miradi mbalimbali inayotekelezwa na Wakala pamoja na kupata elimu kuhusu nishati safi ya kupikia.

Wananchi hao wamepongeza juhudi zinazofanywa na Serikali kupitia REA za kuhakikisha wananchi wanaachana na matumizi ya nishati zisizo safi na salama kwa kupikia.

No comments:

Post a Comment