
Na Okuly Julius, DODOMA
Wizara ya Fedha inashiriki Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2025 yanayofanyika katika Viwanja vya Chinangali, jijini Dodoma kuanzia leo, Juni 16 hadi Juni 23, 2025.
Maadhimisho ya mwaka huu yanaongozwa na kaulimbiu isemayo: “Himiza matumizi ya mifumo ya kidijitali ili kuongeza upatikanaji wa taarifa na kuchagiza uwajibikaji.”
Kupitia ushiriki wake, Wizara ya Fedha inawaalika watumishi wa umma pamoja na wananchi kwa ujumla kutembelea banda lake ili kupata huduma na elimu mbalimbali, ikiwemo elimu juu ya usimamizi wa mali za Serikali na matumizi sahihi ya mifumo ya kidijitali katika sekta ya fedha.




No comments:
Post a Comment