Na Okuly Blog, DODOMA
Katibu wa Siasa na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma, Jawadu Mohamed, amewataka wanasiasa na wananchi kwa ujumla kuepuka lugha za kejeli na dharau dhidi ya wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi, akisisitiza umuhimu wa siasa safi na ushindani wa hoja.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa, Julai 4, 2025 jijini Dodoma, Mohamed amelaani matamshi ya baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani na watu wengine ambayo yanawadhalilisha wagombea, hususan wale wenye asili ya usanii, akisema kauli hizo zinakiuka misingi ya maadili ya kisiasa na ustaarabu wa kidemokrasia.
“Tabia ya kudharau watu kwa kusema wasanii hawafai kugombea ni kinyume cha misingi ya Utanzania wetu. Chama Cha Mapinduzi kinaamini kuwa mwanachama yeyote anayekidhi vigezo vya kikatiba, kikanuni na kimaadili ana haki ya kuchukua fomu na kuomba ridhaa ya chama na hatimaye wananchi kwa ajili ya nafasi yoyote ya uongozi,” amesema.
Jawadu amesema ni muhimu kwa wanasiasa wote kuheshimu wagombea wa vyama vyote, kwani siasa ni jukwaa la ushindani wa hoja, siyo matusi au dharau. Aidha, alitoa wito kwa taasisi za kisiasa na kijamii kuendelea kuhimiza mijadala yenye tija kwa taifa badala ya kuendeleza siasa za kubezana.
“Matamshi haya siyo tu yanadhoofisha maadili ya kisiasa, bali pia yanahatarisha ustawi wa demokrasia yetu ambayo tumeijenga kwa miaka mingi. Tunapaswa kuonesha ukomavu wa kisiasa kwa kuheshimu kila mgombea,” alisisitiza.
Kauli hiyo imekuja wakati ambapo mchakato wa kupokea fomu za uteuzi wa wagombea wa nafasi mbalimbali ndani ya vyama vya siasa ukiendelea nchini kote kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu ujao.

No comments:
Post a Comment