
Naibu Kaibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Chrisian Omolo, akieleza kuhusu umuhimu wa Sera za Kodi kwa maendeleo ya Wananchi, alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha kwenye Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (Sabasaba) yenye kaulimbiu ya “Maonesho ya Kibiashara ya Kimataifa Sabasaba, Fahari ya Tanzania”.. Kulia ni Afisa Kumbukumbu kutoka Kitengo cha Pensheni, Wizara ya Fedha, Bi. Stella Mtally.

Naibu Kaibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Chrisian Omolo, akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Habari wa Wizara hiyo, Bw. Joseph Mahumi kuhusu Jarida la Wizara hiyo (Hazina Yetu) ambalo linapatikana kwa nakala ngumu na Laini, alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha kwenye Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (Sabasaba).

Naibu Kaibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Chrisian Omolo, akikabidhiwa mfuko wenye nembo ya PSPTB na Afisa Uhusiano kwa Umma na Mawasiliano wa Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Bi. Beatrice Sanga, alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha kwenye Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (Sabasaba).

Naibu Kaibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Chrisian Omolo, akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Mwandamizi wa Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali wa Wizara hiyo, Bi. Farida Manilwa Kuhusu elimu ya Pensheni inayotolewa na Hazina alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha kwenye Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (Sabasaba). Katikati ni Afisa Kumbukumbu kutoka Kitengo cha Pensheni, Wizara ya Fedha, Bi. Stella Mtally.

Kaimu Kamishna wa Kitengo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi, Bw. Bashiru Taratibu, akizungumza na wataalamu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha kwenye Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (Sabasaba) yenye kaulimbiu ya “Maonesho ya Kibiashara ya Kimataifa Sabasaba, Fahari ya Tanzania”. Wa pili kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi hiyo, Prof. William Pallangyo.

Kaimu Kamishna wa Kitengo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi, Bw Bashiru Taratibu, akisoma Jarida la Hazina Yetu toleo la Tatu kwa mwaka 2024/2025 baada ya kupata maelezo kutoka kwa Afisa Habari Mkuu kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara hiyo, Bi. Eva Valerian, alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha kwenye Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (Sabasaba) yenye kaulimbiu ya “Maonesho ya Kibiashara ya Kimataifa Sabasaba, Fahari ya Tanzania” .

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Chrisian Omolo, akiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa Wizara ya Fedha wanaotoa elimu alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha kwenye Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (Sabasaba) ambayo yameanza tarehe 28 Juni na kutarajiwa kuhitimishwa Julai 13 mwaka huu.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha)
Na. Peter Haule na Joseph Mahumi , WF, Dar es Salaam
Wananchi wametakiwa kuwa na uelewa kuhusu Sera za Kodi zinazoandaliwa na Wizara ya Fedha kwa lengo la kumfanya mwananchi kulipa kodi kwa hiari ili kuisaidia Serikali kutoa huduma bora na endelevu katika sekta mbalimbali ikiwemo ya afya, maji, barabara, nishati na kilimo.
Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha na mabanda mengine kwenye Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (Sabasaba) ambayo yameanza tarehe 28 Juni na kutarajiwa kuhitimishwa Julai 13 mwaka huu.
Alisema kuwa Bunge limepitisha Bajeti Kuu ya Serikali ya Kiasi cha shilingi trilioni 56.49 ambayo inalenga pamoja na mambo mengine kutekeleza miradi yenye faida ya moja kwa moja kwa mwananchi kama barabara, nishati, maji na kilimo.
Bi. Omolo alisema kuwa jukumu la mwananchi katika kufanikisha hilo ni pamoja na kulipa kodi kwa hiari kwa mazingira rafiki ambayo yanatokana na Sera nzuri za kodi ambazo zimeandaliwa na Wizara ya Fedha.
Ametoa rai kwa wananchi wanaotembelea katika Maonesho hayo kufika Banda la Wizara ya Fedha ili kukutana na wataalamu ambao watawapa elimu ya Sera ya Kodi na faida zake kwa jamii.
Bi. Omolo amewahakikishia wananchi kupata huduma bora kutoka Serikalini kupitia Bajeti iliyopitishwa na Bunge hivi karibuni kwa kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na kwa gharama nafuu.
Aidha, alisema kuwa ndani ya Banda la Wizara ya Fedha inatolewa elimu ya huduma ndogo za fedha kwa lengo la kuhakikisha wananchi wanakuwa na uelewa wa masuala ya fedha ili kuondokana na kuchukua mikopo isiyo na tija.
Alisema pia kuwa Banda la Wizara ya Fedha linashirikisha Vyuo vikuu vilivyo chini ya Wizara ambavyo vinatoa elimu kuhusu kozi mbalimbali ambapo alivitaja vyuo hivyo kuwa ni pamoja na, Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP), Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) na Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA).
Aidha alisema kuwa wataalamu wengine ni kutoka Idara na Vitengo vya Wizara hiyo na Taasisi zake ikiwa ni pamoja na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), Mfuko wa Dhamana na Uwekezaji Tanzania (UTT AMIS), Mfuko wa Self Microfinance, Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) na Soko la Bidhaa Tanzania (TMX).
Taasisi nyingine ni pamoja na Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), Baraza la Masoko ya Mitaji (CMT), Benki ya Maendeleo TIB na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Hazina SACCOS, Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA), Mamlaka ya Rufaa za Zabuni za Umma (PPAA) na Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA).
No comments:
Post a Comment