
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mheshimiwa Dkt Stergomena Lawrence Tax (Mb), tarehe 7 Julai 2025, ameonya na kuwatahadharisha Wanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM, kuwa macho na kujiepusha na makundi au watu wenye nia ovu na Nchi ya Tanzania, watakaotaka kuutumia mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, kuleta vurugu. Dkt. Tax, ameyasema hayo wakati akizungumza na Wajumbe wa CCM kata ya Kandawe, Magu mkoani Mwanza, alipowatembelea katika ziara yake kama Mlezi wa Kata hiyo.
Katika hotuba yake, Waziri Tax amewakumbusha wajumbe hao kujitokeza kwa wingi kupiga kura ili kutimiza haki yao ya kikatiba ya kuwachagua viongozi wanaoamini kuwa watawaletea maendeleo kwa ajili ya Ustawi wao na Taifa kwa ujumla.
Aidha, Ziara hiyo ya kutembelea Kata ya Kandawe, imehudhuriwa pia na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Magu, Komredi Enos Ndobeji Kalambo.













No comments:
Post a Comment