Dkt. Yonazi Akagua maendeleo ya Maandalizi ya Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa 2025 - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, July 19, 2025

Dkt. Yonazi Akagua maendeleo ya Maandalizi ya Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa 2025



Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu, Dkt. Jim Yonazi amefanya ukaguzi wa maandalizi ya kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa yanayotarajiwa kufanyika tarehe 25 Julai, 2025 katika Uwanja wa Mashujaa, Mtumba Jijini Dodoma.

Dkt. yonazi ametembelea na kujionea eneo yatakapofanyika maadhimisho hayo na kupokea taarifa ya maandalizi husika kwa lengo la kuhakikisha Maadhimisho hayo yanafanyika kwa viwango vilivyokusudiwa.

Imeelezwa kuwa mgeni rasmi katika Maadhimisho hayo atakuwa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Aidha kuhusu hali ya maandalizi hayo, imeelezwa kuwa yanaendelea vizuri, huku tukio hilo likitarajiwa kuwa la kitaifa na kihistoria kwa Nchi yetu.








No comments:

Post a Comment