
Kufuatia video fupi iliyokuwa ikisambaa mitandaoni, ikimuonesha mtoto Riziwani Martin Asheri mwenye umri wa miaka 13, mkazi wa Kibaigwa mkoani Dodoma ambaye ana kipaji cha kujenga barabara na madaraja, Waziri wa Ujenzi Abdallah Ulega alituma Maafisa kutoka Wizarani kumtembelea mtoto huyo ili kupata ukweli wa taarifa hiyo.
Maafisa hao walipata fursa ya kuzungumza mengi na mtoto huyo, mama yake, mjomba wake na mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Karume ambapo walieleza mambo kadhaa kuhusu historia ya maisha ya mtoto huyo kwa ujumla na elimu yake.
Pia walielezwa kuhusu ndoto za mtoto huyo ambaye anatamani akiwa mkubwa aje kuwa mhandisi mkubwa nchini atakayeleta maendeleo kupitia sekta ya Ujenzi.








No comments:
Post a Comment