"NIKIWA RAIS KIMA CHA CHINI CHA MSHAHARA NI MILIONI MOJA NA LAKI TANO - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, July 10, 2025

"NIKIWA RAIS KIMA CHA CHINI CHA MSHAHARA NI MILIONI MOJA NA LAKI TANO


Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia Makini, Ameir Hassan Ameir, amesema kuwa chama hicho kimejipanga kuhakikisha kinainua uchumi wa wananchi, ikiwa ni pamoja na kutangaza kima cha chini cha mshahara kuwa Shilingi milioni 1.5 kwa mwezi.

Ameir ameyasema hayo wakati akizungumza na vyombo vya habari katika mjadala wa wazi uliowakutanisha viongozi wa dini, wawakilishi wa vyama vya siasa, na waandishi wa habari.

Amesema Chama cha Demokrasia Makini kina mpango wa kutangaza sera madhubuti, hasa katika eneo la kuinua uchumi wa wafanyakazi, na kusisitiza kuwa chama hicho kitaweka maslahi ya wananchi mbele katika kila hatua ya utekelezaji wa sera zake.

No comments:

Post a Comment