SERIKALI YA AWAMU YA SITA YAING'ARISHA KAGERA SEKTA YA AFYA NA ELIMU - MWASSA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, July 1, 2025

SERIKALI YA AWAMU YA SITA YAING'ARISHA KAGERA SEKTA YA AFYA NA ELIMU - MWASSA


MKUU wa Mkoa wa Kagera Hajjat Fatma Mwassa akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 1,2025 jijini Dodoma , kuhusu mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika Mkoa huo.


Na Okuly Julius ,Dodoma


MKUU wa Mkoa wa Kagera Hajjat Fatma Mwassa, amesema katika kipindi cha Novemba 2020 hadi Aprili 2025, jumla ya shilingi bilioni 146.3 zimetumika katika sekta ya afya mkoani humo.

Amesema hali hiyo imesababisha ongezeko la vituo vya kutolea huduma za afya kutoka 249 hadi 336. Hospitali zimeongezeka kutoka tatu (3) hadi 11, vituo vya afya kutoka 29 hadi 42 na zahanati kutoka 217 hadi 283.

Mwasa ameyasema hayo leo Julai 1,2025 jijini Dodoma wakati akieleza mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika Mkoa huo wa Kagera

Ambapo amesema hospitali mpya za wilaya nane zimejengwa, na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa imeongeza huduma za kibingwa tano zikiwemo upasuaji wa masikio, koo, pua, mifupa na magonjwa ya ndani. Huduma hizi zimepunguza kwa kiasi kikubwa rufaa kwenda hospitali za mikoa ya jirani na Taifa.

“Idadi ya wagonjwa waliotibiwa ndani ya mkoa kwa huduma za kibingwa imeongezeka kutoka 128,305 hadi 478,002, ongezeko la asilimia 273,” amesema Mwassa.

Amesema katika kipindi hicho, upatikanaji wa dawa umeimarika kutoka asilimia 85 hadi 93, huku vifaa tiba vya kisasa kama CT-Scan, ECHO na ECG vikiwa vimefungwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa. Idadi ya watumishi wa afya imeongezeka kutoka 2,139 hadi 3,542 na nyumba za watumishi zimefikia 423 kutoka 318.

Kwa upande wa sekta ya elimu, Mwasa amesema serikali imetumia zaidi ya shilingi bilioni 128 kuboresha miundombinu ya shule, vyuo vya mafunzo na ajira za walimu. Shule za awali na msingi zimeongezeka kutoka 942 hadi 1,058, wakati shule za sekondari zimeongezeka kutoka 224 hadi 292, zikiwemo shule tatu za amali na shule mpya ya bweni ya wasichana – Kagera River – iliyogharimu zaidi ya bilioni 4.1.

"Vyuo vya VETA vimeongezeka kutoka 4 hadi 9, kikiwemo Chuo cha VETA cha Mkoa cha Burugo kilichojengwa kwa zaidi ya bilioni 20. Ujenzi wa Kampasi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mkoani Kagera umefikia asilimia 70 ya utekelezaji," ameeleza Mwassa

Aidha, vyumba vya madarasa vimeongezeka kwa 4,709 kutoka 9,596 hadi 14,305, wakati maabara za sayansi zimeongezeka kutoka 346 hadi 513. Mabweni yamefikia 203 kutoka 82, na walimu wapya 1,610 wameajiriwa katika shule za msingi na sekondari.

Kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi wa sekondari kimeongezeka kutoka asilimia 91.0 hadi 94.57, hatua inayotajwa kuwa matokeo ya uwekezaji mkubwa katika elimu.

Mkuu huyo wa Mkoa amesema mafanikio hayo yanaweka msingi imara kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi mkoani Kagera, huku viongozi wakiahidi kuendeleza kasi hiyo katika sekta nyingine ikiwemo maji, kilimo, nishati na uwekezaji.


No comments:

Post a Comment