TAARIFA KWA UMMA UPUNGUFU WA MAJI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Sunday, July 13, 2025

TAARIFA KWA UMMA UPUNGUFU WA MAJI


Ndugu Mteja na Mdau wetu tunaomba radhi, kutakuwa na Upungufu wa Maji kwa siku mbili kuanzia Leo siku ya Jumapili tarehe 13 Julai, 2025 hadi siku ya Jumatatu tarehe 14 Julai, 2025. Upungufu huo wa Maji umetokana na hitilafu kwenye pump ya kisima namba C-1 kilichopo Mzakwe chenye uwezo wa kuzalisha lita za maji 7,200,000 kwa siku, ambapo hitilafu hiyo imetokea leo tarehe 13 Julai, 2025.

Maeneo yote yenye mgao wa maji kwa siku ya Leo na Kesho yataathirika kwa kupata maji pungufu Ndugu mteja, Huduma ya maji itaanza kurejea kesho mchana Jumatatu tarehe 14 Julai, 2025, baada ya matengenezo kukamilika.

DUWASA inaomba radhi wateja wake kwa usumbufu uliyojitokeza. Kwa Mawasiliano zaidi, tafadhali usisite kuwasiliana nasi kwa simu namba 0800110078 bure. Imetolewa na: Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma - DUWASA 13.07.2025

No comments:

Post a Comment