Afisa Usalama wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga, Paul Maisori akizungumza kwenye mkutano wa TANESCO na viongozi wa madereva wa bodaboda wa Manispaa ya Shinyanga

Afisa Usalama wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga, Paul Maisori akizungumza kwenye mkutano wa TANESCO na viongozi wa madereva wa bodaboda wa Manispaa ya Shinyanga kwa lengo la kujadili mikakati ya kuimarisha ulinzi na usalama wa miundombinu ya umeme.
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Shinyanga limekutana na viongozi wa madereva wa bodaboda wa Manispaa ya Shinyanga kwa lengo la kujadili mikakati ya kuimarisha ulinzi na usalama wa miundombinu ya umeme.
Mkutano huo umefanyika Julai 20,2025 katika Viwanja vya Mazingira Center, Mjini Shinyanga, ukiongozwa na Afisa Usalama wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga, Paul Maisori, ambaye amesisitiza kuwa waendesha bodaboda wana nafasi kubwa katika kulinda miundombinu hiyo muhimu ya taifa.
Maisori amesema Mkutano huo ni sehemu ya jitihada za TANESCO kuimarisha uhusiano na jamii katika kuhakikisha usalama wa miundombinu ya umeme unaimarika, sambamba na kuhamasisha matumizi salama ya nishati hiyo muhimu.
"Waendesha bodaboda ni walinzi wetu wa kwanza. Tunataka kuwa na ushirikiano wa karibu nanyi. Mkiona mtu anahujumu au kubeba nyaya za TANESCO, toeni taarifa mapema. Tunalinda wasiri wetu na tunatoa zawadi kwa wanaotoa taarifa za uhujumu,” amesema Maisori.
Maisori ameongeza kuwa TANESCO ina dhamira ya kuhakikisha umeme unapatikana kwa uhakika kwa wananchi, hivyo kila mwananchi anatakiwa kuwa mlinzi wa miundombinu hiyo ikiwemo transfoma na nguzo za umeme, ambazo huchimbwa mchanga karibu nazo hali inayotishia usalama.
Kwa upande wake, Afisa Mahusiano na Huduma kwa Wateja wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga, Emma Nyaki, amewakumbusha wananchi kuwa wanaweza kuwasiliana na shirika hilo bila gharama kupitia namba ya simu bure 180, muda wowote.
“Tupo tayari kupokea taarifa na kutoa msaada kwa wananchi. Lengo letu ni kuhakikisha huduma ya umeme inapatikana kwa usalama na ufanisi,” amesema Nyaki.
Viongozi wa madereva bodaboda wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha Madereva na Wamiliki wa Pikipiki Tanzania (CHAMWAPITA) Wilaya ya Shinyanga Mjini, Mohamed Juma Mlabbu wameishukuru TANESCO kwa elimu hiyo na kuahidi kutoa ushirikiano kwa vitendo.
“Tumejifunza mengi. Tuko tayari kushirikiana na TANESCO kulinda miundombinu ya umeme kwa maendeleo ya wananchi na taifa,” amesema Mlabbu.

Afisa Usalama wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga, Paul Maisori akizungumza kwenye mkutano wa TANESCO na viongozi wa madereva wa bodaboda wa Manispaa ya Shinyanga

Afisa Usalama wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga, Paul Maisori akizungumza kwenye mkutano wa TANESCO na viongozi wa madereva wa bodaboda wa Manispaa ya Shinyanga

Afisa Mahusiano na Huduma kwa Wateja wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga, Emma Nyaki akizungumza kwenye mkutano wa TANESCO na viongozi wa madereva wa bodaboda wa Manispaa ya Shinyanga

Mwenyekiti wa Chama cha Madereva na Wamiliki wa Pikipiki Tanzania (CHAMWAPITA) Wilaya ya Shinyanga Mjini, Mohamed Juma Mlabbu akizungumza kwenye mkutano wa TANESCO na viongozi wa madereva wa bodaboda wa Manispaa ya Shinyanga

No comments:
Post a Comment