UBIA WA BARRICK NA TWIGA WAZIDI KUSTAWISHA UCHUMI NA THAMANI YA PAMOJA NCHINI TANZANIA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, July 7, 2025

UBIA WA BARRICK NA TWIGA WAZIDI KUSTAWISHA UCHUMI NA THAMANI YA PAMOJA NCHINI TANZANIA

 

Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari Julai 7,2025 katika Mgodi wa Barrick Bulyanhulu - Picha : Kadama Malunde
Rais na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Barrick, Mark Bristow akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari Julai 7,2025 katika Mgodi wa Barrick Bulyanhulu.

***
Serikali imepongeza uwekezaji mkubwa uliofanywa na Kampuni ya Barrick inayoendesha shughuli zake nchini kwa ubia na Serikali kupitia kampuni ya Twiga katika kipindi cha miaka mitano kwa kuwa unachagia kwa kiasi kikubwa katika pato la Taifa na kunufaisha wananchi.

Akiongea na waandishi wa habari mgodini Bulyanhulu, Julai 7,2025 Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa, amesema ubia huu ni wa mfano wa kuigwa katika uwekezaji nchini kwa kuwa mafanikio yake ni makubwa na migodi ya Twiga na Barrick inaendeshwa kwa weledi mkubwa na kutumia teknolojia za kisasa zenye kuleta tija na ufanisi na kuchangia ukuaji wa uchumi wa kijamii nchini kwa ujumla.
Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa

Kwa upande wake, Rais na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Barrick, Mark Bristow, amesema ubia huo umejenga mfano endelevu wa uendelezaji wa rasilimali madini nchini tangu uanzishwe na na kuipa sura mpya nafasi ya sekta ya madini katika maendeleo ya taifa, ukizidi kuongeza thamani ya pamoja, ubora wa kiuendeshaji na uwekezaji wa muda mrefu kwa mustakabali wa nchi.

“Tulipoanzisha Twiga, lengo lilikuwa zaidi ya kusuluhisha changamoto za kihistoria. Lilikuwa kujenga mustakabali mpya kwa kuufungua utajiri wa dhahabu wa Tanzania kwa njia inayogawanya kwa haki manufaa yake na kujenga thamani ya kudumu kwa wadau wote. Baada ya miaka mitano, tumeirejesha Barrick katika hali ya kuwa mchangiaji mkubwa katika uchumi wa nchi kwenye sekta hii, huku tukitambuliwa kitaifa katika nyanja mbalimbali kuanzia usalama, matumizi ya bidhaa na huduma za ndani, hadi elimu na miundombinu,” amesema Bristow.


Tangu Barrick ichukue rasmi jukumu la uendeshaji wa migodi mbalimbali nchini mnamo mwaka 2019, kampuni hiyo imeingiza dola bilioni 4.79 katika uchumi wa Tanzania, ikiwa ni pamoja na dola milioni 558 katika nusu ya kwanza ya mwaka 2025 pekee. Zaidi ya asilimia 90 ya ununuzi wa bidhaa na huduma umeendelea kufanyika kutoka kampuni za Kitanzania, ambapo nyingi kati ya hizo ni za wazawa, huku asilimia 95 ya wafanyakazi wake wakiwa Watanzania na asilimia 49 wakitoka katika jamii zinazozunguka migodi.
Rais na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Barrick, Mark Bristow.

Mfano wa kuigwa wa hatua zinazochukuliwa na ubia wa Twiga ni Mpango wa Kusongesha Mbele Mustakabali wa Elimu, ambao ni uwekezaji wa pamoja wa dola milioni 30 kati ya Barrick na Serikali ya Tanzania kupitia Ofisi ya Rais, unaolenga kupanua miundombinu ya shule nchini. Mpango huu, sasa ukiwa katika awamu ya pili, unatarajiwa kuwapatia vyumba vya madarasa wanafunzi zaidi ya 45,000.

Migodi ya Barrick nchini Tanzania imeendelea kutoa uzalishaji kulingana na makadirio. Katika mgodi wa Bulyanhulu, utengenezaji wa njia ya chini kwa chini katika eneo la Magharibi Juu umepiga hatua kubwa ya maendeleo yakiimarishwa na ujio wa mitambo mipya na upanuzi wa miundombinu. Uwekezaji maalumu kwenye mifumo ya uingizaji hewa na upunguzaji maji umeboresha ufanisi, kuondoa vikwazo na kuuwezesha mgodi kuzalisha dhahabu zaidi kwa miongo ijayo.

Katika mgodi wa North Mara, mfumo mpya wa kuhifadhi umeme kwa betri uliozinduliwa hivi karibuni umesaidia kuboresha upatikanaji wa nishati, huku shughuli za uchimbaji chini ya ardhi na kwenye machimbo ya wazi zikiendelea kama zilivyopangwa. Shughuli za kuwahamisha watu makazi zimekaribia kukamilika, na Barrick inaendelea kujenga imani na kukubalika kwa uendeshaji wa shughuli zake katika jamii.

“Ushirikiano wetu na jamii zinazotuzunguka ni msingi wa kuwepo kwetu nchini Tanzania. Tumelazimika kufanya kazi kwa bidii ili kuurejesha uhusiano huo, hususan katika eneo la North Mara, na sasa tunaona matokeo chanya ya mawasiliano endelevu na utekelezaji wa ahadi zetu,” amesema Bristow.

Wakati huohuo, Barrick inaendelea kuwekeza kikamilifu katika utafutaji wa madini katika maeneo mapya ya uchimbaji ili kuhakikisha uendelevu wa mustakabali wa shughuli zake nchini. Programu za uchorongaji zinaendelea kulenga kuongeza hifadhi ya madini katika maeneo ya Gokona na Gena ndani ya mgodi wa North Mara, na katika miamba ya Tabaka la aina ya 1 na Tabaka la aina ya 2 katika eneo la Bulyanhulu. Pia, ufuatiliaji na uchorongaji wa kijiofizikia kwa kutumia njia ya upepo umepangwa kufanyika katika maeneo mapya ya Siga na Nzega.

Hata katika mgodi wa Buzwagi, ambao sasa uko katika hatua ya kufungwa, jitihada zinaendelea kuelekezwa katika kuleta thamani ya muda mrefu. Ukanda Maalumu wa Kiuchumi unaandaliwa katika eneo hilo, huku wawekezaji kadhaa wakiwa tayari wameonesha nia. Chuo cha Barrick kinatarajiwa kutoa mafunzo kwa wasimamizi na mafomeni zaidi ya 2,800 kutoka maeneo mbalimbali ifikapo mwishoni mwa mwaka huu, hivyo kuendeleza mchango wa Barrick katika kukuza vipaji vya sekta ya madini barani Afrika.

“Dhamira yetu kwa Tanzania haikukoma pale mawe ya dhahabu yalipoisha kule Buzwagi. Tunaacha tumeweka miundombinu na taasisi zitakazonufaisha taifa kwa muda mrefu ujao,” amesema Bristow.

Akihitimisha maelezo yake kuhusu safari ya miaka mitano ya Twiga, Bristow amesema ubia huo haukusaidia tu kurejesha utulivu wa uendeshaji wa migodi bali pia umejenga msingi wa ustawishaji wa thamani ya muda mrefu kupitia umiliki wa pamoja, uwezeshaji wa wenyeji, na mkabala wa kiuwajibikaji wa kuleta maendeleo.

“Twiga ni zaidi ya kampuni; ni mfano wa kile ambacho sekta ya madini inaweza kuwa pale shughuli zinapotekelezwa kwa usahihi, kwa ubia na kwa malengo,” amehitimisha.
Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari Julai 7,2025 katika Mgodi wa Barrick Bulyanhulu
Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari Julai 7,2025 katika Mgodi wa Barrick Bulyanhulu
Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari Julai 7,2025 katika Mgodi wa Barrick Bulyanhulu
Rais na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Barrick, Mark Bristow akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari Julai 7,2025 katika Mgodi wa Barrick Bulyanhulu.
Rais na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Barrick, Mark Bristow akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari Julai 7,2025 katika Mgodi wa Barrick Bulyanhulu.
Rais na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Barrick, Mark Bristow akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari Julai 7,2025 katika Mgodi wa Barrick Bulyanhulu.
Rais na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Barrick, Mark Bristow akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari Julai 7,2025 katika Mgodi wa Barrick Bulyanhulu
Rais na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Barrick, Mark Bristow akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari Julai 7,2025 katika Mgodi wa Barrick Bulyanhulu.
Meneja wa Barrick nchini Dkt. Melkiory Ngido akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari Julai 7,2025 katika Mgodi wa Barrick Bulyanhulu.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Frank Mkinda akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari Julai 7,2025 katika Mgodi wa Barrick Bulyanhulu.


No comments:

Post a Comment