WAGENI WATAKA KUFUATA MFUMO WA TANZANIA KUKABILI MAJANGA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, July 11, 2025

WAGENI WATAKA KUFUATA MFUMO WA TANZANIA KUKABILI MAJANGA



UJUMBE wa wataalamu kutoka nchi za Ghana, Togo na Burkina Faso wamesema wataitumia mifumo ya ufuatiliaji wa majanga na utoaji wa tahadhari za mapema waliyojifunza nchini Tanzania ili kukabiliana na majanga katika nchi zao.

Wataalamu hao wameeleza hayo leo jijini Dodoma wakati wa mafunzo maalum ya mifumo ya ufuatiliaji wa majanga na tahadhari za mapema yaliyoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kupunguza Hatari za Majanga (UNDRR) pamoja na Kituo cha Sayansi cha Afrika Magharibi kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (WASCAL). Mafunzo hayo yamefanyika katika Kituo cha Operesheni na Mawasiliano ya Dharura kilichopo Mji wa Serikali, Mtumba.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu – Sera, Bunge na Uratibu, Brigedia Jenerali Hosea Ndagala amesema uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan katika mifumo ya usimamizi wa maafa umechangia kwa kiasi kikubwa kupunguza madhara ya majanga nchini.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Msaidizi wa Kituo cha Operesheni na Mawasiliano ya Dharura, Jane Kikunya, amesema mafunzo hayo yamekuwa na manufaa makubwa baada ya wataalamu hao kutoka nchi za Afrika Magharibi kuonesha nia ya kufunga mifumo hiyo katika nchi zao ili kusaidia ufuatiliaji wa majanga na utoaji wa tahadhari kwa wananchi.









No comments:

Post a Comment