WASHIRIKA WA MAENDELEO KUCHANGIA SH. BILIONI 161 MFUKO WA AFYA WA PAMOJA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, July 19, 2025

WASHIRIKA WA MAENDELEO KUCHANGIA SH. BILIONI 161 MFUKO WA AFYA WA PAMOJA


Waziri wa Afya, Mhe. Jenista Mhagama na Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dkt. Festo Dugange, wakishuhudia Makatibu Wakuu wa Wizara ya Fedha, TAMISEMI na Afya, wakisaini Hati ya Makubaliano na Washirika wa Maendeleo ya kuchangia kiasi cha Shilingi bilioni 161 katika Mfuko wa Afya wa Pamoja, jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El- maamry Mwamba na wadau wengine, wakisaini Hati Hati za Makubaliano ya kuchangia kiasi cha Shilingi Bilioni 161.3 kwenye Mfuko wa Afya wa Pamoja (Health Basket Fund) kutoka kwa Washirika wa Maendeleo, wakati wa hafla ya kusainiwa kwa makubaliano hayo, jijini Dar es Salaam. Kulia nyuma ni Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dkt. Festo Dugange akishuhudia.

Makatibu Wakuu wa Wizara ya Fedha, TAMISEMI, Afya na Washirika wa Maendeleo wakionesha Hati ya Makubaliano ya kuchangia kiasi cha shilingi bilioni 161 katika Mfuko wa Afya wa Pamoja, baada ya kusainiwa jijini Dar es Salaam, wakishuhudiwa na Waziri wa Afya, Mhe. Jenista Mhagama na Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dkt. Festo Dugange.

Waziri wa Afya, Mhe. Jenista Mhagama akimkabidhi zawadi Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuwahudumia Watoto (UNICEF), Mhe. Elke Wisch, baada ya kusainiwa kwa Hati ya Makubaliano ya kuchangia kiasi cha shilingi bilioni 161 katika Mfuko wa Afya wa Pamoja, wa pili kushoto ni Naibu Waziri TAMISEMI, Dkt. Festo Dugange, kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba na kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Dkt. Seif Shekalaghe.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El- maamry Mwamba, akiwapongeza wadau wa maendeleo kwa kusaini Hati za Makubaliano ya kuchangia kiasi cha Shilingi Bilioni 161.3 kwenye Mfuko wa Afya wa Pamoja (Health Basket Fund) kutoka kwa Washirika wa Maendeleo, wakati wa hafla ya kusainiwa kwa makubaliano hayo, jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El- maamry Mwamba (kushoto), akiteta jambo na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais TAMISEMI, Bw. Adolf Ndunguru, kabla ya kusainiawa kwa Hati za Makubaliano ya kuchangia kiasi cha Shilingi Bilioni 161.3 kutoka kwa Washirika wa Maendeleo kwenye Mfuko wa Afya wa Pamoja (Health Basket Fund), wakati wa hafla ya kusainiwa kwa makubaliano hayo, jijini Dar es Salaam.

Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuwahudumia Watoto (UNICEF), Mhe. Elke Wisch, akiipongeza Tanzania kwa jitihada zake katika kusimamia makubaliano katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Sekta ya Afya, wakati wa kusainiawa kwa Hati za Makubaliano ya kuchangia kiasi cha Shilingi Bilioni 161.3 kutoka kwa Washirika wa Maendeleo kwenye Mfuko wa Afya wa Pamoja (Health Basket Fund), jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Afya, Mhe. Jenista Mhagama na Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dkt. Festo Dugange wakiwa katika picha ya pamoja na Makatibu Wakuu, Wizara ya Fedha, TAMISEMI, Afya na Wadau wa maendeleo baada ya kusainiawa kwa Hati za Makubaliano ya kuchangia kiasi cha Shilingi Bilioni 161.3 kutoka kwa Washirika wa Maendeleo kwenye Mfuko wa Afya wa Pamoja (Health Basket Fund), jijini Dar es Salaam.


(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha)


Na. Peter Haule, WF, Dar es Salaam


Serikali ya Tanzania na washirika wa Maendeleo wanaochangia Mfuko wa Afya wa Pamoja (Health Basket Fund), wamesaini Hati ya makubaliano ya kuchangia katika Mfuko huo kiasi cha dola za Marekani milioni 55.86 sawa na shilingi za Tanzania bilioni 161.33 kwa mwaka wa fedha 2025/26.

Hafla ya kusainiwa kwa Hati ya Makubaliano hayo imefanyika jijini Dar es Salaam kati ya Makatibu Wakuu wa Wizara ya Fedha, TAMISEMI na Wizara ya Afya na Washirika wa Maendeleo, wakishuhudiwa na Waziri wa Afya, Mhe. Jenista Mhagama na Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dkt. Festo Dugange.

Akizungumza kwa niaba ya Makatibu Wakuu hao, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha ambaye pia ndiye Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Natu El- Maamry Mwamba alisema kuwa makubaliano hayo ya uchangiaji wa fedha kwenye Mfuko wa Pamoja wa Afya ni matokeo ya ushirikiano wa dhati katika kuisaidia sekta ya Afya.

Alisema kuwa misaada hiyo ni mwendelezo wa makubaliano ambayo yalisainiwa mwaka 2021 na yanatarajiwa kumalizika Julai Mosi, 2026 ambapo yataandaliwa makubaliano mengine.

Dkt. Mwamba alisema, kwa niaba ya Wizara ya Fedha na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anawashukuru Washirika hao kwa msaada ambao utasaidia katika juhudi za kuboresha sekta ya Afya.

Alisema kuwa vipaumbele vya misaada hiyo, vinaenda sambamba na vipaumbele vya nchi katika Sekta ya Afya na si katika kukuza sekta hiyo pekee lakini pia misaada hiyo inachochea maendeleo kwa wananchi wengi katika nyanja mbalimbali.

Dkt. Mwamba amewataja Washirika wa Maendeleo waliochangia katika Mfuko wa Pamoja wa Afya kuwa ni pamoja na Serikali ya Switzerland, Ireland, Canada, Uingereza, Denmark, Korea, Shirika la Kimataifa la Kuwahudumia Watoto (UNICEF), Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA) na Benki ya Dunia.


Dkt. Mwamba ameahidi kuwa kila msaada utakaotolewa utatumika kwa uwazi na kwa lengo lililokusudiwa ili kuwa na matokeo tarajiwa.

No comments:

Post a Comment