DKT. ASHATU KIJAJI: NIPO TAYARI KULIPA DENI KWA WANANCHI WA KONDOA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, August 25, 2025

DKT. ASHATU KIJAJI: NIPO TAYARI KULIPA DENI KWA WANANCHI WA KONDOA



Mgombea wa Ubunge wa Jimbo la Kondoa kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Ashatu Kijaji, amesema anatambua kuwa bado ana deni kubwa kwa wananchi wa jimbo hilo na ameahidi kulilipa kwa kufanya kazi kwa bidii, usiku na mchana endapo atapewa tena ridhaa ya kuwatumikia katika nafasi hiyo.

Dkt. Ashatu ameyasema hiyo leo Agosti 25, 2025 mara baada ya kukabidhiwa rasmi fomu ya uteuzi wa kugombea Ubunge na Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Kondoa, kutoka Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, mkoani Dodoma.

Makabidhiano hayo ni sehemu ya maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 unaotarajiwa kufanyika tarehe 29 Oktoba mwaka huu.

Kadhalika, Dkt. Ashatu amewashukuru Viongozi wa juu wa chama cha Mapinduzi (CCM) kwa imani waliyoionesha kwake kwa kumteua tena kuwa mgombea wa Ubunge kupitia chama hicho.

Amemshukuru kwa namna ya kipekee Mwenyekiti wa CCM Taifa, Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kwa kumteua kupeperusha bendera ya chama katika uchaguzi huo.

“Nawashukuru kwa dhati viongozi wa chama changu kwa kuniamini tena. Najua bado nina deni kwa wananchi wa Kondoa, naahidi kulilipa kwa kufanya kazi kwa juhudi na maarifa usiku na mchana.” amesema Dkt. Ashatu







No comments:

Post a Comment