KAMPENI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA YARUDISHA UOTO WA ASILI NJOMBE - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, August 21, 2025

KAMPENI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA YARUDISHA UOTO WA ASILI NJOMBE


Bodi ya Nishita Vijijini (REB) imefuraishwa na kupongeza hatua za baadhi ya Magereza nchini kuanza kurudisha mazingira katika hali yake ya uoto wa asili baada ya magereza hayo kuacha kutumia kuni na mkaa kupikia na kuanza kutumia nishati safi ya kupikia.

Pongezi hizo zimetolewa leo Agosti 21, 2025 na Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Florian Haule wakati wa ugawaji wa mitungi ya gesi ya kilogramu 15 pamoja na majiko ya sahani mbili 232 kwa Watumishi wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Njombe unaotekelezwa na Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

“Kwanza niwapongeze kwa kutambua tuliharibu misitu huko nyuma na tuna wajibu wa kuirudishia. Ninatamani programu kama hii ya upandaji na utunzaji miti unaofanywa na gereza la Wilaya la Njombe uigwe na magereza nyingine zote nchini,” amesema Haule.

Kwa upande wake Mjumbe wa Bodi hiyo, Stephen Mwakifwamba amesema utunzaji wa huo wa miti uliofanywa na magereza Mkoa wa Njombe unapaswa kuigwa na taasisi zingine za serikali na jamii kwa ujumla ili kurejesha uoto wa asili.

Kwa upande wake Mhandishi Emmanuel Yesaya akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati vijijini (REA), amesema zaidi ya hekta 470 zinakatwa kila mwaka kwa ajili ya matumizi ya nishati zisizo safi za kupikia huku watanzania zaidi elfu 33 wanafariki kutoka na matumizi ya nishati zisizo safi za kupikia.

Kwa upande wake Mkuu wa Magereza Mkoa wa Njombe, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Joseph Mkude amewataka maafisa pamoja na askari wa jeshi hilo kuwa mabalozi wa nishati safi ya kupikia.

No comments:

Post a Comment