MATAIFA YA AFRIKA MASHARIKI KUUNGANA KUKOMESHA UVUVI HARAMU BAHARI YA HINDI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, August 26, 2025

MATAIFA YA AFRIKA MASHARIKI KUUNGANA KUKOMESHA UVUVI HARAMU BAHARI YA HINDI




Dar es Salaam, Tanzania – 25 Agosti 2025

Mataifa ya Afrika Mashariki yanajiandaa kuchukua hatua madhubuti za pamoja dhidi ya uvuvi haramu, usioripotiwa na usiodhibitiwa (IUUF) katika Bahari ya Hindi ya Kusini Magharibi kupitia Kongamano la Blue Voices (Sauti za Buluu), litakalofanyika jijini Dar es Salaam siku ya Jumatatu, 1 Septemba 2025, kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 6:00 mchana.

Kongamano hili lenye kauli mbiu ya “Kubadili Uelekeo: Hatua za Kikanda Dhidi ya Uvuvi Haramu” limenadaliwa na kuratibiwa na shirika la Ascending Africa chini ya mradi wa, na litawakutanisha viongozi wa serikali, mashirika ya kikanda, watafiti, wabunifu wa kiteknolojia, viongozi wa jamii, mashirika yasiyo ya kiserikali na sekta binafsi.

Uvuvi haramu umegeuka kuwa janga kubwa la kiuchumi na kimazingira. Kila mwaka, mataifa ya Afrika Mashariki yanapoteza zaidi ya Dola za Marekani milioni 415 kutokana na uhalifu huu wa majini. Nchini Tanzania pekee, hasara inafikia takribani Dola milioni 142.8, huku nchini Kenya asilimia 30–40 ya samaki wote wakivuliwa kinyume cha sheria.

“Uvuvi haramu si tu unaharibu mazingira ya baharini, bali pia unalinyonya taifa letu na kuathiri mamilioni ya familia za pwani zinazotegemea bahari kwa kipato na chakula,” alisema Michael Mallya, Msemaji wa Mradi wa Jahazi. “Huu ni uvamizi wa moja kwa moja wa rasilimali zetu na uhuru wetu wa kitaifa. Ni wajibu wetu kuchukua hatua thabiti sasa.”

Kongamano litajikita katika:
- Kuchambua ukubwa na athari za uvuvi haramu katika Tanzania na ukanda mzima.

Kuimarisha mshikamano wa kikanda kati ya nchi za Afrika Mashariki na nchi za ukanda wa Kusini Magharibi mwa Bahari ya Hindi. Nchi hizo ni kama Tanzania, Kenya, Msumbiji, Comoro, Madagascar na Mauritius.

Kujadili mageuzi ya sera, teknolojia bunifu za ulinzi wa bahari, na usimamizi madhubuti wa mipaka ya baharini.
- Kujenga ajenda ya pamoja ya utekelezaji na ahadi za muda mrefu za kulinda rasilimali na mifumo ikolojia ya bahari.

Washiriki wote kutoka sekta za uhifadhi wa bahari, usimamizi wa uvuvi, usalama wa bahari, ustawi wa pwani na uvumbuzi wa kiteknolojia wanakaribishwa kushiriki.

Usajili na Mawasiliano:
Jisajili kupitia: https://jahaziproject.org/blue-voices-roundtable-virtual-registration

Kwa mawasiliano zaidi:
Michael Mallya
Msemaji wa Mradi wa Jahazi
+255 789 147 255
michael.mallya@jahaziproject.org

No comments:

Post a Comment