BARRICK BULYANHULU YALETA FURAHA NYANG’HWALE KWA KUFANIKISHA UJENZI WA SHULE YA MCHEPUO WA KIINGEREZA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, September 4, 2025

BARRICK BULYANHULU YALETA FURAHA NYANG’HWALE KWA KUFANIKISHA UJENZI WA SHULE YA MCHEPUO WA KIINGEREZA

 

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Ismail Ali Ussi (kushoto) akizindua jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa madarasa katika shule ya Kharumwa
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Ismail Ali Ussi  (kushoto) akizindua jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa madarasa katika shule ya Kharumwa
Muonekano wa sehemu ya madarasa
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Ismail Ali Ussi akizungumza wakati wa hafla hiyo
Mkuu wa wilaya ya Nyang'hwale Grace Kingalame akiongea katika hafla hiyo

Katika dhamira yake ya kuboresha miundo mbinu ya elimu ili kuwawezesha watoto wa Kitanzania kusomea katika mazingira bora, Kampuni ya Barrick nchini yenye ubia na Serikali kupitia mgodi wake wa Bulyanhulu imeendelea kuboresha mazingira ya kusomea ya shule ya msingi mpya ya Serikali ya mchepuo wa Kiingereza ya Kharumwa iliyopo wilayani Nyang’hwale mkoani Geita ambayo ilijengwa kwa fedha za uwajibikaji kwa jamii (CSR).

Katika kipindi cha mwaka huu halmashauri ya wilaya ya Nyang’hwale imepata Shilingi milioni 100,996,200 kwa ajili ya kutekeleza ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa na kununua samani kwa ajili ya kuondoa changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa.

Akiongea wakati wa kupokea mwenge ulioambatana na kuweka jiwe la msingi la Katika shule hiyo, Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru, Ismail Ali Ussi ameipongeza Barrick kwa kuendelea kuunga mkono jitihaza za Serikali za kuboresha maisha ya wananchi kupitia uwezeshaji wa miradi katika sekta mbalimbali za maendeleo ikiwemo elimu.

“Nachukua fursa hii kuwapongeza wataalamu wote wa Halmashauri na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa kufanya kazi usiku na mchana katika kuhakikisha Watanzania wananufaika na miradi mbalimbali inayotekelezwa katika Wilaya hii. Natoa wito kwa wananchi wa wilaya hii waleteni watoto shule hakuna tena kisingizio cha umbali wa shule, shule zinajengwa kila sehemu na hii inatokana na Ushirikiano wa serikali pamoja na wadau kama Barrick , hakika Barrick mnazidi kumheshimisha Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan” ,amesema Ussi.

Mkuu wa Wilaya ya Nyang’hwale, Mhe.Grace Kingalame amesisitiza umuhimu wa kufanya kazi kwa bidii na kuendelea na ari hiyo ya kutekeleza miradi ya huduma za wananchi kwa viwango vya juu ili kukidhi mahitaji ya wananchi.

Mwakilishi wa Barrick katika hafla hiyo, Samson Mashala ambaye ni Afisa Uhusiano wa jamii katika mgodi wa Bulyanhulu amesema mgodi utaendelea kufanya kazi na Serikali kuhakikisha miradi ya CSR iliyoibuliwa na wananchi inatekelezwa kwa viwango na kuboresha maisha ya wananchi.

No comments:

Post a Comment