
Mgombea Mwenza wa Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi akiwahutubia Wakazi wa mji mdogo wa Isaka wilayani Kahama, jimbo la Msalala,kwenye mkutano mdogo wa hadhara leo Alhamis Septemba 3,2025,mkoani Shinyanga.
Pamoja na mambo mengine Dkt Nchimbi pia aliwanadi wagombea Ubunge,akiwemo Mgombea Ubunge wa Jimbo la Msalala Mabula Johnson Magangila pamoja na Madiwani.
Balozi Dkt.Emmanuel Nchimbi anaendelea na mikutano yake ya Kampeni Mkoani Shinyanga ya kuinadi Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu 2025-2030,ambayo inalenga kuboresha maisha ya wananchi na ustawi wa Maendeleo katika miaka mitano ijayo huku akitumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi kumchagua mgombea Urais wa CCM,Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan, Wabunge na Madiwani wa Chama hicho kwa kura za kishindo ifikapo Oktoba 29,2025.









No comments:
Post a Comment