DK.NCHIMBI APOKEA BARUA YA MKAZI WA BUKOBA MJINI MWENYE ULEMAVU WA MIGUU. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Sunday, September 7, 2025

DK.NCHIMBI APOKEA BARUA YA MKAZI WA BUKOBA MJINI MWENYE ULEMAVU WA MIGUU.


MGOMBEA mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi akimsikiliza Mlemavu wa Miguu,Amos Kalungula.

Dk.Nchimbi yuko mkoani Kagera ambako amewasili tangu jana na leo Septemba 7 ameendelea na mikutano ya kampeni ya kuomba kura za Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 29,2025.

Akiwa katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Kashai Bukoba Mjini baada ya kuwahutubia wananchi,alimfuata Kalungula ambaye ni mlemavu wa miguu aliyekuwa ameshika bahasha yenye rangi ya kaki na kisha kumkabidhi Dk.Nchimbi.

Hata hivyo bahasha hiyo aliyokabidhiwa Dk.Nchimbi haijafahamika ilikuwa imebeba ujumbe gani .Hata hivyo mkazi huyo alionekana kufurahishwa na upendo ulioneshwa na Dk.Nchimbi aliyeamua kumfuata kumsikiliza na kupokea barua hiyo.


No comments:

Post a Comment