Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ameungana na mamia ya waombolezaji kutoa pole kwa familia ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi kufuatia kifo cha kaka yake Abass Mwinyi ambaye pia alikuwa mgombea Ubunge wa Jimbo la Fuoni kilichotokea Zanzibar, Unguja usiku wa kuamkia Septemba 25, 2025.
Dkt. Biteko ameshiriki mazishi hayo Septemba 26, 2025 Bumbubwini Mangapwani, Zanzibar.
Ambapo ameungana na viongozi mbalimbali akiwemo Mgombea Mwenza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa, Ndugu Stephen Wasira, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla .
Aidha, baada ya mazishi baadhi viongozi walipata fursa ya kutoa heshima katika kaburi la Hayati Ali Hassan mwinyi lililopo Bumbubwini Mangapwani, Zanzibar.
Awali, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan alifika msibani kuwafariji wafiwa na kisha kusaini kitabu cha maombolezo.

No comments:
Post a Comment