WAHANDISI WANAOKIUKA MAADILI KUCHUKULIWA HATUA: ULEGA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, September 26, 2025

WAHANDISI WANAOKIUKA MAADILI KUCHUKULIWA HATUA: ULEGA



Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega ameitaka Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB) kuwachukulia hatua za kinidhamu na kutopewa kazi nyingine wahandisi wasiofanya kazi zao kwa uadilifu na wasiozingatia viapo na miiko ya taaluma yao.

Ameeleza hayo Septemba 26, 2025 jijini Dar es Salaam wakati akifunga maadhimisho ya 22 ya Siku ya Wahandisi Tanzania ambayo yamebebwa na kauli mbiu “Wajibu wa Wahandisi kuelekea Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050”.

Amewaeleza wahandisi kuwa makini na viapo hivyo kwani miradi isiyotekelezwa vyema na wahandisi inaharibu taswira ya taaluma, inahatarisha usalama na wakati mwingine hupoteza rasilimali na imani ya wananchi.

Amepongeza Bodi kwa kuandaa utaratibu wa utoaji zawadi kwa wanafunzi wanaochipukia kwa kuwapa hamasa na kutambua jitihada wanazozifanya ili kuwatia moyo katika kuendeleza taaluma hiyo na hivyo kuwataka ERB kutanua wigo na kushirikisha wadau mbalimbali ili kudhamini utoaji wa tuzo hizo

Aidha, ameiagiza ERB kuwasilisha Wizarani mapendekezo yote yaliyotokana na mkutano huo kwa ajili ya utekelezaji ili kufikia malengo na kuleta maendeleo ya kiuchumi katika nchi yetu.

Maadhimisho ya mwaka huu yameshirikisha zaidi ya wahandisi 4,000 kutoka ndani na nje ya nchi ikiwemo washiriki kutoka India, Ethiopia, Uganda na Kenya huku wahandisi wapatao 400 wakila kiapo cha utiifu.






No comments:

Post a Comment